2030 (wimbo)
2030 ni jina la wimbo uliotungwa na kuimbwa na msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Roma Mkatoliki. Wimbo ulirekodiwa mnamo mwaka wa 2012 kupitia studio ya Tongwe Records chini ya utayarishaji wake Jay Rider. Kama jinsi ilivyo kawaida ya Roma, wimbo unalenga masuala ya kijamii zaidi kuliko habari za starehe. Maelezo ya ndani yanabashiri au kutazamia namna Tanzania ya 2030 jinsi itakavyo kuwa. Hasa anaponda sera za serikali ya CCM namna inavyoendesha nchi na huu mmong'onyoko wa udini unaoendelea kuikumba Tanzania kwa kipindi hiki.
"2030" | ||
---|---|---|
Wimbo wa Roma Mkatoliki | ||
Umetolewa | 2012/2013 January, 2013 | |
Umerekodiwa | 2012 | |
Aina ya wimbo | Hip-hop ya Tanzania | |
Lugha | Kiswahili | |
Urefu | 6:30 | |
Studio | Tongwe Records | |
Mtunzi | Roma Mkatoliki | |
Mtayarishaji | Jay Rider |
Katika wimbo, ametaja mauaji ya Mapadri na Masheikhe. Hina haja ya kutukana Quran wala Biblia. Anaimba kwa amani zote kuhakikisha ya kwamba haiegemei upande wa mtu yeyote ndani yake.
Viungo vya Nje
hariri- Roma 2030 katika YouTube
- Wimbo Huu katika blogu ya Hass-Baby Ilihifadhiwa 5 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.