Abbah Process

Mwanamuziki wa Tanzania

Sweetbert Charles Mwinula (Abbah process) (amezaliwa 28 July 1994) ni mwanamuziki na muandaaji wa muziki nchini Tanzania. [1][2] Alijizolea umaarufu mwingi kupitia kazi zake ambazo aliziandaa na ambazo ameshirikishwa na alizofanya yeye mwenyewe, kwa mfano "Maisha na Muziki" ya Darassa[3], "Chibonge" ya Marioo, Bytarbeast na Abbah. Hizo ni baaadhi ya kazi ambazo alizifanya zikampatia umaarufu na kupelekea kushindanishwa kwenye vinyang'anyiro mbalimbali Afrika. [4]

Abbah Process
Jina la kuzaliwa Sweetbert charless mwinula
Pia anajulikana kama Abbah Process,The hit monster
Asili yake Tanzania
Aina ya muziki Hiphop, Bongo_Fleva,R&B
Kazi yake Mwanamuziki na Muandaaji wa Muziki
Ala R&B
Miaka ya kazi 15
Studio Abbah Music
Ame/Wameshirikiana na Harmonize, Mauasama, Darassa, Sho Madjozi, Richmavoko
Tovuti https://abbah-music.com
Ala maarufu
R&B
Abbah Process.

Historia hariri

Abbah alizaliwa mkoa wa Dar es Salaam hospitali ya Amana, na tangu akiwa mdogo alipendelea kupiga ala za muziki. Baada ya kumaliza masomo yake akajikita rasmi kwenye tasnia ya muziki, na mwaka 2015 alifanikiwa kumiliki studio yake mwenyewe. Hapo aliweza kuwasaidia vijana wengi wa Kitanzania kufikia malengo yao, kwa kuchukua vijana wenye vipaji vichanga na kuviendeleza zaidi. Alimsaidia Marioo, Bytar, Kapipo na the MixKiller. [5]

Abbah alifanikiwa kujizolea umaarufu katika nchi za jirani na Tanzania ambazo ni Kenya na Uganda.

Abbah Music hariri

Mnamo mwaka 2019 Abbah alifungua kampuni ya Muziki, yenye makao yake jijini Dar es Salaam; kampuni hiyo inajikita kwenye masuala ya uandaaji wa muziki, usimamizi wa kazi za wasanii, usimamizi wa wasanii, kituo cha kufundisha uandaaji muziki. Kupitia kampuni hiyo na vijana aliowafunza waliweza kutoa mchango mkubwa ikiwa wamewashirikisha wasabi nguli kutoka Afrika, kama Burna Boy, Morgan Heritage, Yemi Alade na wengine wengi.

Abbah anajulikana kama mtengeneza beats mbaya zaidi. Yeye hufanya beats kwa nyota na ujao. Takriban 40% ya nyimbo maarufu sasa Abbah alizitengeneza. Blessings ni wimbo aliomshirikisha mkali wa RnB Jux, ambao unafanya kuwa moja ya nyimbo bora zaidi mitaani kwa sasa. [6]

Tanbihi hariri

  1. Abbah Lyrics, Biography and Videos | Afrika Lyrics. afrikalyrics.com. Iliwekwa mnamo 2020-05-11.
  2. "Music of Tanzania", Wikipedia (in English), 2020-04-13, retrieved 2020-05-11 
  3. ONE ON ONE: Darassa (en). Daily Nation. Iliwekwa mnamo 2020-05-11.
  4. Victor Kileo TZA. List kamili ya washindi wa tuzo za Sound City MVP 2020 – Millardayo.com (en-US). millardayo.com. Iliwekwa mnamo 2020-05-11.
  5. Producer Abbah amtambulisha msanii mpya Bytar, afananishwa na Burna Boy (Video) (en-US). Bongo5.com (2020-04-07). Iliwekwa mnamo 2020-05-11.
  6. https://offblogmedia.com/audio-abbah-feat-jux-blessings-download-mp3/

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Abbah Process kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.