Ad Turres (Byzacena)

Turres ilikuwa mji katika Jimbo la Afrika ya Kiroma, baadaye Jimbo la Byzacena na katika Milki ya Wavandali katika Tunisia ya leo. Eneo lake na magofu ya mji wa kale yanaaminiwa kuwa karibu na Tamarza kwenye mpaka wa Algeria.[1]

Eneo kwenye oasisi ya Tamarza; majiranukta kwenye ramani: 34°23′N 7°57′E / 34.38°N 7.95°E / 34.38; 7.95

Tamarza ni oasisi kwenye milima penye maji mazuri takriban kilomita 70 kutoka mji wa Tozeur[2].

Turres ilikuwa mji mwenye askofu wakati wa Dola la Roma na majina ya maaskofu wawili yamehifadhiwa katika kumbumubu ya historia. Tangu mwaka 1933 Kanisa Katoliki limeanza kutumia tena jina la Turres kama dayosisi ya jina kwa ajili ya maaskofu wasio na dayosisi halisi.[3][4]

Marejeo

hariri
  1. Titular Episcopal See of Turres in Byzacena, GCatholic.org.
  2. Tamarza, Baclays Travel 2014
  3. Le Petit Episcopologe, Issue 127.
  4. Revue des Ordinations Épiscopales, Issue 1955, Number 71.