Afrika ya Kiroma

Africa ilikuwa jimbo la Kiroma kwenye mwambao wa Mediteranea. Eneo lake lilikuwa takriban Tunisia ya kaskazini pamoja na pwani la Libya ya magharibi.

Sarafu ya Kaisari Hadrian iliyotolewa kwa heshima ya jimbo la Africa. Mtu ambaye ni mfano wa Africa avaa kofia ya tembo.
Dola la Roma mnamo 120 BK; jimbo la Afrika kwa rangi nyekundu

Miji muhimu ilikuwa Karthago na Leptis Magna. Jimbo lilikuwa maarufu kama "ghala ya ngano" ya Roma.

Bara la Afrika lilipokea jina lake kutoka jimbo hili. Waarabu waliendelea kutawala eneo lake kwa jina la jimbo la Ifriqiya amabalo ni matamshi yao ya "Afrika".