Tunisia (kirefu: Jamhuri ya Tunisia - kwa Kiarabu الجمهرية التونسية, al-Jumhūrīya at-Tūnisīya) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini inayopakana na Bahari ya Mediteranea, Libya na Algeria.

الجمهورية التونسية
al-Jumhūriyya at-Tūnisiyya
Jamhuri ya Tunisia
Bendera ya Tunisia Nembo ya Tunisia
Wimbo wa Taifa Humata l-hima
Lugha rasmi Kiarabu
Mji mkuu Tunis
Aina ya serikali Jamhuri
Rais Kais Saied
Waziri Mkuu Ahmed Hachani
Eneo km² 163.610
Wakazi 11,708,370 (Julai 2020)
Wakazi kwa km² 71.65
Uhuru 20 Machi 1956 (kutoka Ufaransa)
Pesa Dinari ya Tunisia
Wakati UTC +1
Sikukuu ya Taifa 7 Novemba
Tunisia katika Afrika ya Kaskazini
Tunisia katika Afrika ya Kaskazini
Ramani ya Tunisia

Nchi imegawanyika katika mikoa 6 tena katika wilaya 24.

Mji mkuu ni Tunis (wakazi 1,066,961) ulioko mahali pa Karthago ya kale.

Historia hariri

Tunisia iliwahi kutawaliwa na Wafinikia walioanzisha huko mji wa Karthago.

Baada ya hao kushindwa na Roma ya Kale, ilikuwa jimbo la Afrika katika Dola la Roma.

Kisha eneo lake likatawaliwa kwa awamu na Wavandali, Waarabu, Wahispania, Waturuki na Wafaransa.

Tarehe 20 Machi 1956 ilipata uhuru.

Watu hariri

Wakazi karibu wote (98%) wanajiita Waarabu na hutumia lugha ya Kiarabu ambacho ndicho lugha rasmi. Hata hivyo damu yao ni mchanganyiko hasa wa ile ya Waberber, Waarabu na Waturuki.

Takriban watu 200,000, hasa kusini, wanaendelea kuzungumza Kiberber ambacho ni lugha asili ya wenyeji lakini Waberber wengi wamezoea kutumia Kiarabu.

Katika elimu na biashara Kifaransa kinatumika pia sana.

Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na asilimia 99 za wakazi, nao ndio dini rasmi, lakini theluthi moja kati yao, na nusu kati ya vijana, wanajitambulisha kama wasio na dini, kiwango kikubwa kuliko nchi zote za Kiarabu. Waliobaki ni Wakristo, hasa Wakatoliki, na Wayahudi wachache.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tunisia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.