Afande Sele

Mwanamuziki wa Tanzania

Seleman Msindi au Afande Sele (alizaliwa tar. 24 Aprili 1976) ni msanii wa muziki wa hip hop na Bongo Flava kutoka Mkoani Morogoro, Tanzania. Amewahi kushinda tuzo ya (mkali wa ryhmes) mwaka 2003 kutokana na wimbo yake wa "Darubini Kali" aliyomshirikisha Dogo Ditto kwa sasa Lameck Ditto. Ni muasisi wa makundi ya 'Ghetto Boys' na 'Watu Pori', yaliyoanzishwa na kufia mjini Morogoro kwa kuongozana na alikuwa msanii wa kwanza kuujaza uwanja wa mpira wa miguu wa JAMUHURI mjini morogoro alipozindua albam yake ya kwanza ya 'MKUKI MOYONI'. Aliongoza kampeni ya maleria mwanzoni mwamiaka ya 2005 na 2007.

Seleman Msindi

Amezaliwa Seleman Msindi
24 april 1976
Morogoro
Nchi Tanzania
Majina mengine Afande Sele
Kazi yake Mwanamuziki

Mwanzoni wa mwezi wa 11 mwaka 2012 alitangaza rasmi kufanya kazi kama kundi jipya la watu pori baada ya kufanya kazi na MC KOBA ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wakiunda kundi la watu pori miaka ya nyuma. Ametoa Nyimbo nyingi kali ikiwemo MTAZAMO, Amani Na Upendo, SIMBA DUME Na nyingine nyingi.Afande Sele kwa sasa ana video ya wimbo wake Soma Ule ambayo imeongozwa na mtayarishaji Raph Tz (upcoming video director) aliyepewa heshima na msanii huyo kufanya video hiyo ambayo imekidhi maudhui ya wimbo.

Maisha Binafsi hariri

Afande Sele ana watoto wawili wa kike, Tunda na Sanaa wanaishi huko mkoani Morogoro. Afande Sele alifiwa na mkewe Asha (Mama Tunda) mnamo Agosti 14, 2014. Kwa sasa Tunda anasoma sekondari iitwayo Charlotte iliyopo maeneo ya nanenane, mkoani Morogoro.

Afande Sele kwa sasa amejiunga na chama cha Alliance for Change Tanzania (ACT) ambacho kinaongozwa na aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Zuberi Kabwe. Hapa alikuwa akitokea CHADEMA. Huku nako hakudumu sana akajivua uanachama wake na kuhamia Chama cha Mapinduzi.[1]

Marejeo hariri

  1. "Afande Sele atangaza kujiunga na CCM, Aeleza sababu - Bongo5.com", Bongo5.com (in en-US), 2018-03-15, retrieved 2018-07-05 
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Afande Sele kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.