Afya na mwonekano wa Michael Jackson

Michael Jackson (29 Agosti 1958 – 25 Juni 2009) alikuwa mwanamuziki na mburudishaji wa Kimarekani ambaye ametumia zaidi ya miaka arobaini katika jicho la umma, kwanza akiwa kama nyota mtoto akiwa na kundi zima la The Jackson 5, kishaa badaaye kama msanii wa kujitegemea. Kuanzia katikati mwa miaka ya 1980 imekuwa wazi kwamba mwonekano wa Jackson ulikuwa unabadilika bila kificho. Ngozi ya mwili wake imeanza kupauka, pua na umbo la sura yake imebadilika, na kapoteza uzito.

Michael Jackson in the White House's Diplomatic Reception Room in Mei 1984.

Ile hali ya mpauko wa ngozi awali ulisababishwa na vitiligo na lupus (ugonjwa wa ngozi ambao tiba yake ni tata) — ambao Jackson alijaribu kuutibia kunako mwaka wa 1986—na matumizi yake ya vipodozi mbalimbali ili kuficha madoa yake ya mwilini.[1] Baadhi ya madaktari wa upasuaji wamekisia ya kwamba pia alifanya "rhinoplasty" (upasuaji wa pua), kuinua paji la uso, upasuaji na usawazishaji wa kidevu, na kabadilisha vilevile midomo yake.[2] Hayo yote ya karibu yanakadiliwa kufanywa na mwimbaji huyo kunako miaka ya 1990, amepitia karibia michakato kumi ya kubadili umbo lake.[1]

Jackson na baadhi ya ndugu zake walisema ya kwamba walikuwa wakinyanyasika sana kimwili na kihisia na baba yao, na mwaka wa 2003, alikubali kwamba alikuwa akimchapa viboko sana Jackson wakati yu mtoto.[3] Jackson hapendi kabisa kulizungumzia hili, lakini pindi tu anapolisema, anakuwa na huzuni sana na kusema ya kwamba angetapika kabla ya kukutana na baba'ke. Madaktari wanasema alikuwa na matatizo ya maumivu ya mwili. Deepak Chopra, daktari na rafiki wa karibu Jackson kwa karibia miaka 20, amesema: "Kilichokuwa shurutisho kwake ni hali ya kufanya upasuaji uliokuwa a hali ya kujibalisha mwenyewe, hali ambayo dhahiri ni kutojiheshimu au kujikubali wewe kama wewe."[4]

Wakati fulani katika miaka ya 1990, ilionekana ya kwamba Jackson amekuwa tegemezi kubwa la madawa mbalimbali, hasa dawa za kuua maumivu na na vipoozeo vikalivikali, na afya yake ikaanza kuyumba waziwazi. Ameenda kujiswafi kunako mwaka wa 1993 kwa msaada wa Elizabeth Taylor na Elton John,[5] lakini ulevi wa dawa ulibaki palepale. Amefariki kwa mshtuko wa moyo kunako tar. 25 Juni 2009.

Vitiligo na lupus, tiba na athari

hariri
 
Jackson miaka miwili baada ya kubainiwa kuwa ana vitiligo, picha imepigwa wakati wa hatua za awali za ugonjwa huo

Ngozi ya Jackson ilikuwa rangi ya kahawia (au sana huita maji ya kunde) katika hali ya ujana wake, ila, kuanzia katikati mwa miaka ya 1980, hatua kwa hatua ngozi yake ikaanza kudhoofika mno kwa kile kilichofikiriwa kujichubua ngozi na kujibadilisha mwonekano wake kuwa Mzungu. Mabadiliko haya yalienea katika kila chombo cha habari.[6] Kwa mujibu wa wasifu wa J. Randy Taraborrelli, mnamo 1986, Jackson alifanyiwa tiba ya vitiligo na lupus; vitiligo yenyewe tu tayari ishafanya ngozi iwe nyeupe, na lupus ilikuwa inaishia; magonjwa yote mawili yalikuwa yanamfanya akimbie mwanga wa jua, kitendo ambacho kilisababisha hali ya ugonjwa wake wa lupus kurudi upya.[1]

Kutibu hali hizi, Jackson akatumia Solaquin, Tretinoin (dawa ya kutibu utangoutango mixa vipele) na Benoquin. Vilevile alikuwa na kawaida ya kutumia hydroxychloroquine kwa kujichoma moja kwa moja katika jelaha lake la kichwani.[1] Tiba alizokuwa anatumia kwa ajili ya hali yake ilikuwa inaongeza zaidi kupausha ngozi yake, na kamchezo kake cha kujipaka madawa ya kuoanisha weupe wa ngozi yake imezidi kumfanya aonekane kituko.[1]

Mnamo mwezi wa Februari ya mwaka wa 1993, Jackson ametoa uwazi usio wa kawaida katika mahojiano yake ya dakika tisini na Oprah Winfrey, mahojiano yake ya kwanza televisheni tangu mwaka wa 1979. Wakati wa mahojiano haya, amelikataa swali la kwamba anajichubua, katangaza kinagaubaga ya kwamba alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa vitiligo na kwa maana hiyo ametumia dawa kadhaa wa kadhaa kuhakikisha hiyo hali inamuondoka.Mahojiano hayo yalitazamwa na watu milioni 62 kutoka Marekani.[7] Hoja ya vitiligo imezua gumzo katika jamii, hali ambayo ilikuwa haijulikani hapo awali.[6][8][9][10] Uchunguzi wa maiti ya Jackson umethibitisha kuwa alikuwa na vitiligo.[11]

Wakati wa kufanya ziara ya Kiaustralia ya HIStory World Tour, Jackson akamuoa mwuguzi wake wa masuala ya ugonjwa wa ngozi Bi. Debbie Rowe.[12][13] Wawili hao walikutana katikati mwa miaka ya 1980, wakati Jackson alivyokuwa anatibiwa ugonjwa wa vitiligo. Ametumia miaka mingi kutibu ugonjwa wake vilevile kutoa misaada ya kihisia na kifikra, na wakajenga uhusiano mkubwa kabla hawajaanzisha mahusiano ya kimapenzi.[14] Wawili hao walitalikiana mnamo mwaka wa 1999 na wakabaki marafi tangu hapo.[15]

Utaratibu wa vipodozi na mpangalio wa mlo

hariri
 
Jackson akiwa katika tamasha la 1997 Cannes Film Festival.

Umbo la sura yake limebadilika pia; madaktari wa upasuaji kadhaa wamekisia ya kwamba, kunako miaka ya 1990, amepitia upasuaji kadhaa wa pua, kuinua paji la uso, kufanya midomo iwe myembaba, na upasuaji wa mfupashavu.[2] Kulingana na mwana-wasifu J. Randy Taraborrelli, Jackson alifanya upasuaji wake wa pua kwa mara ya kwanza baada ya kuvunja pua yake wakati anacheza mchezo wa hatari kunako mwaka wa 1979.

Hata hivyo, upasuaji huo haukukamilika kisawasawa, na kulalamika ya kwamba upumuaji wake wa tabu utaathiri shughuli zake. Akaelekezwa kwa Dk. Steven Hoefflin, ambaye alifanya upasuaji wake wa pua wa pili mnamo mwaka wa 1981.[16] Katherine Jackson, ingawa, alisema hivi karibuni katika mahojiano yake ya kwamba Michael alipata madhila yake ya pua kwa makusudi hapo mara ya kwanza. Taraborrelli alieleza kwamba Jackson alifanya tena upasuaji wa pua kwa mara ya tatu miaka mitatu baadaye na ya nne mnamo mwaka wa 1986.[17]

Jackson ameandika katika tawasifu wake mnamo 1988 Moonwalk kwamba, katika ongezeko la upasuaji wa pua, pia alipata kutengeneza kidimpo katika kidevu chake.[18] Toka 1986 na kuendelea alikuwa mteja wa kawaida wa Arnold Klein, a mtaalamu wa magonjwa ya ngozi ambaye amebobea katika tiba ya sindano za ugonjwa ngozi, utaratibu wa utoaji wa tiba ya upodozi bila upasuaji.[19]

Katika kitabu chake, Jackson amedhania kuwa madailiko ya sura yake ni matokeo ya kubalehe, mpangalio mkali wa mlo wa kutokula nyma, upungufu wa uzito, badiliko katika mtindo wa nyewele na mataa ya jukwaani.[18] Jackson amekana madai ya kwamba kabadilisha macho yake.[20] Kunako 1990, kiwango chote cha upasuaji wa Jackson kilijadiliwa mno; hayo yalikaribia kusema kwamba mwimbaji huyo amepitia karibia taratibu kumi za upasuaji katika sura yake tu hadi sasa.[1] Ilivyofika mwezi Juni 1992, gazeti la Daily Mirror limeweka picha nzima katika ukurasa wake wa mbele, likidai sura ya Jackson, ambayo walielezea kama "sura mbaya isiyo na umbo zuri" kwa kufanya upasuaji wa sura.

Jackson akalishtaki jarida hilo na mwaka wa 1998 wakakubaliana kuondoa kesi mahakamani na kuyamaliza na Jackson. Wakiwa Mahakama Kuu, mhariri wa zamani wa gazeti hilo alitoa taarifa baada ya kukutana na Jackson ana-kwa-ana, na kuamini kwamba Jackson hakuwa na sura la kutisha wala yeye mwenyewe hatishi kabisa. Mwasheria wa Daily Mirror amesawazisha chapisho kwa kusema kwamba toleo lile halijagongana na picha.[21]

Afya wasiwasi

hariri

Utoto na matatizo ya akili

hariri

Jackson na baadhi ya ndugu zake walieleza ya kwamba walikuwa wakinyanyaswa na kudhalilishwa sana na baba yao Joseph wakati wapo wadogo, kupitia mazoezi ya kila siku, viboko na matumizi ya kuitana majina mabaya ya kashfa kama vile "nyampua" kwa Jackson; udhalilishaji huu umemwathiri Jackson kwa maisha yake yote.[22] Katika moja ya mabishano makali—ambayo baadaye yalikumbushiwa na Marlon Jackson—Joseph alimning'iniza Michael miguu juu kichwa chini huku akimshika mguu mmoja tu na "kumchapa vibiko kwa mkono wake tena na tena, na kumpiga vibako vya matakoni".[23] Joseph alikuwa na kawaida ya kuwachukua vijana na kuwatupa ukutani.[23]

Usiku mmoja wakati Jackson kalala, Joseph amepanda hadi chumbani kwa mwanae kwa kupitia dirilisha la bafuni. Huku akiwa amevaa kinyago cha kutisha, ameingia chumbani na kuanza kupiga ukelele wa nguvu. Joseph amesema eti alitaka kuwafundisha watoto zake wasiache dirisha wazi wakati wanaenda kulala. Kwa miaka kadhaa baada ya hapo, Jackson amesumbuliwa na ndoto za kutisha za jinamizi linakuja kumchukua chumbani kwake.[23] Mwanzoni mwa miaka ya 1980, alikuwa hana furaha kabisa; Jackson alieleza, "Hata nyumbani, nipo mpweke. Ninakaa chumbani kwangu na wakati mwingine najililia mwenyewe. Ni vigumu sana kuwa na marafiki... Wakati mwingine natoka nje wakati wa usiku na kuzungukia maeneo ya jirani, nikiwa na matumani ya kumpata japo mtu wa kuzungumza nae. Lakini naishia kurudi nyumbani."[24]

Ijapokuwa ilikuwa imeripotiwa kudhalilishwa kwake wakati yupo mtoto kwa miaka kadhaa, yeye binafsi alizungumza kinagaubaga kuhusu hilo katika mahojiano yake ya mwaka wa 1993 na Oprah Winfrey. Alikunja uso kwa huzuni wakati anazungumzia mateso aliyokuwa ana pata kutoka katika mikono ya baba yake mzazi; na aliamini ya kwamba ameyakosa maisha yake ya utotoni kwa miaka kadhaa, akikubaliana na hali ya kwamba alikuwa akilia mara kwa mara hasa kwa kufuatia upweke aliokuwa nao.[6][8][9] Katika mahojiano yaleyale, kuhusu baba'ke, Jackson alisema, "Kulikuwa na wakati alikuwa anakuja kuniona, napata homa... Naanza kucheua. Samahani... Tafadhali usinikasirikie... Lakini nampenda."[25] Katika mahojiano mengine ya Jackson yenye maudhui ya hali ya juu ya Living with Michael Jackson (2003), Jackson alificha uso wake na kuanza kulia pale anapozungumzia maisha ya utotoni mwake na mateso aliyokuwa anayapata.[23]

Jackson alikumbushia kwamba Joseph alikuwa ana-kaa katika wakati kundi linafanya mazoezi, na kusema, "Akiwa na mkanda mkono mwake. Kama hujafanya chapchap, lazima akupe kubwa, na akikupa lazima uisikie - sio mchezo. Ilikuwa ovyo kishenzi. Ovyo kwelikweli nakwambia."[26] Mwaka wa 2003, mwimbaji huyu alishtakiwa kwa kosa la udhalilishaji wa watoto kesi iliisha baada ya miaka miwili. Wakati uchuguzi unaendelea, hali ya Jackson ilishughulikiwa na Stan Katz, mtaalamu wa masuala ya akili, ambaye pia alitumia masaa kadhaa na mshitaki. Kwa mujibu wa J. Randy Taraborrelli, uchunguzi uliofanywa na Katz ulionesha Jackson akili yake imerudi kama mtoto mwenye miaka kumi.[27] Baadhi ya wataalamu wa tiba walithubutu kusema hadharani kwamba wanaamini mwimbaji pia alikuwa na matatizo ya akili ya kujiona kama watu wengine wanamwona si yeye kutaka mwonekano wa mtu mwingine, hali ya kisaikolojia ambapo msumbuliwa hana wazo au uwezo wa kufikiria taswira yake jinsi watu wanavyochukulia.[1]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 Taraborrelli, pp. 434–436
  2. 2.0 2.1 "Surgeon: Michael Jackson A 'Nasal Cripple'". ABC News. 8 Februari 2003. Iliwekwa mnamo Nov. 11, 2006. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  3. Can Michael Jackson's demons be explained?, BBC News, 27 Juni 2009.
  4. Posner, Gerald. Deepak Chopra: How Michael Jackson Could Have Been Saved, The Daily Beast, 2 Julai 2009.
  5. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named campbell (1995) 89-93
  6. 6.0 6.1 6.2 Campbell (1995), pp. 14–16
  7. "Thriller for Diane Sawyer: Interview with Jackson Two", Daily News, 18 Mei 1995. Retrieved on Jul. 3, 2009. Archived from the original on 2020-04-10. 
  8. 8.0 8.1 Lewis pp. 165–168
  9. 9.0 9.1 George, pp. 45–46
  10. 'I'm a black man turning white on television'", BrisbaneTimes, 18 Desemba 2007
  11. Siemaszko, Corky. "Michael Jackson autopsy report confirms singer suffered from vitiligo, wore wig, had tattooed makeup", Daily News, 10 Februari 2010. Retrieved on Jun. 25, 2010. Archived from the original on 2012-06-11. 
  12. Taraborrelli, pp. 580–581
  13. Taraborrelli, p. 597
  14. Taraborrelli, p. 570
  15. Taraborrelli, pp. 599–600
  16. Taraborrelli, pp. 205–210
  17. "How Jackson's surgery was a desperate bid not to look like the father he hated", Mail Online, 2009-07-01. Retrieved on 2012-04-08. 
  18. 18.0 18.1 Jackson, pp. 229–230
  19. "CNN.com", CNN. 
  20. Jackson, p. 256
  21. "Mirror says sorry for Jackson libel", BBC, 9 Novemba 1998. Retrieved on Jul. 29, 2008. 
  22. "Michael Jackson's Secret Childhood". VH1. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-15. Iliwekwa mnamo Jun. 20, 2008. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  23. 23.0 23.1 23.2 23.3 Taraborrelli, pp. 20–22
  24. Taraborrelli, p. 206
  25. Taraborrelli, p. 620
  26. Taraborrelli, p. 602
  27. Taraborrelli, p. 648

Soma zaidi

hariri