Oprah Winfrey
Oprah Winfrey (jina la kuzaliwa Orpah Gail Winfrey; alizaliwa 29 Januari 1954) ni mjasiriamali wa media, mwigizaji, mtayarishaji, na mfadhili nchini Marekani. Winfrey anajulikana zaidi kwa kipindi chake cha runinga anapoongea na wageni wake kinachojulikana kama Oprah Winfrey Show chenye watazamaji wengi.
Oprah Winfrey | |
---|---|
Makazi | Montecito, California, U.S. Lavallette, New Jersey, U.S. Telluride, Colorado, U.S. Maui, Hawaii, U.S. Chicago, Illinois, U.S. Fisher Island, Florida, U.S. |
Pia aliigiza katika filamu kadhaa zikiwa ni pamoja na The Colour Purple, The Butler na A wrinkle in time. [1]
Maisha ya awali
Winfrey alizaliwa mnamo Januari 29, 1954 huko Kosciusko, Mississippi. Aliitwa "Orpah" kwa jina la mhusika katika Kitabu cha Ruthu. Watu walimwita "Oprah" kwa kosa, akaamua kukubali jina hilo na kulitumia.
Mama yake, Vernita Lee, aliyefanya kazi ya mtumishi kwenye nyumba za watu, alimzaa wakati hajiolewa. Vernita alishindwa kumlea, kwa hiyo aliishi miaka kadhaa kwa bibi yake na baadaye aliishi kwa muda na baba yake, Vernon Winfrey.
Alipata mimba alipokuwa na miaka 14 lakini mtoto wa kiume alizaliwa mapema akafa mara moja. Aliposoma shule ya sekondari alianza tayari kusoma habari kwenye kituo cha redio. Mwaka 1971 alipokewa katika mradi wa msaada wa masomo kwenye Chuo Kikuu cha Tennessee aliposoma mawasiliano.
Alianza kufanya kazi katika redio na runinga huko Nashville. Alishiriki vipindi vya runinga huko Baltimore na Chicago. [1]
Onyesho la Oprah Winfrey
Mnamo 1986, alipata kipindi chake cha pekee cha Oprah Winfrey Show. Watazamaji walimpenda kwa utu alioonyesha akiongea na wageni wake kuhusu maisha yao. Idadi ya watazamaji ilikuwa kubwa na hatimaye Oprah aliweza kununa haki za kipindi hicho.
Mtandao wa Oprah Winfrey
Winfrey sasa anaendesha Mtandao wa Oprah Winfrey. Mnamo Januari 15, 2008, Mawasiliano ya Winfrey na Ugunduzi yalitangaza mipango ya kubadilisha Channel ya Afya ya Ugunduzi kuwa chaneli mpya inayoitwa OWN: Oprah Winfrey Network. Ilipangwa kuzinduliwa mnamo 2009, lakini ilichelewa, na ilizinduliwa mnamo Januari 1, 2011. Yeye pia mwenyeji wa onyesho Sura ijayo ya Oprah kwenye mtandao. [2]
Maisha binafsi
Winfrey alikuwa na mahusiano mbalimbali wa kimapenzi lakini hakuolewa. Tangu mwaka 1986 ameendelea na Stedman Graham. Kutokana na biashara yake ya media na mauzo ya vitabu ametajirika. Mwaka 2013, alitajwa kuwa mmoja wa watu tajiri 400 katika Marekani. Ndiye Mmarekani mweusi pekee katika kundi hilo. [3] Winfrey hufadhili miradi mingi, kwa mfano amegharimia elimu wasichana nchini Afrika Kusini. Kwa ajili ya uhisani wake alitunukiwa medali ya Uhuru wa Rais na Barack Obama mnamo 2013 na digrii ya heshima kutoka kwa Harvard .
Alimkubali Barack Obama mnamo 2006 kwa uchaguzi wa 2008. Makadirio fulani yalisema yalipiga kura milioni moja katika mbio za msingi za kidemokrasia za 2008.
Marejeo
- ↑ 1.0 1.1 "Oprah Winfrey". A+E Television Networks LLC. Iliwekwa mnamo 10/16/2013.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help) - ↑ "Oprah's Next Chapter - OWN TV". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-01-13. Iliwekwa mnamo Januari 12, 2012.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Everything's Coming Up Oprah: How Winfrey Got Richer in 2013
Tovuti nyingine
- Tovuti rasmi ya Oprah Winfrey
- Oprah Winfrey
- Oprah Winfrey
- NPR "Oprah: Kila Mkazi wa Bilionea". Faili ya sauti, video na wasifu . Kupatikana Septemba 17, 2010
- Works by Oprah Winfrey
- Video ya Oprah Winfrey Ilihifadhiwa 16 Februari 2013 kwenye Wayback Machine. iliyotengenezwa na Watunga: Wanawake Wanaotengeneza Amerika
- Winfrey Appearances
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Oprah Winfrey kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |