Akili bandia ya kuzalisha

Akili bandia ya kuzalisha, akili bandia inayozalisha, akili bandia zalishaji au akili bandia zalishi (kwa Kiingereza: generative artificial intelligence, generative AI, GenAI au GAI kwa kifupi) ni akili bandia yenye uwezo wa kuzalisha maandishi, picha, sauti, au video kwa kutumia mitandao ya neva bandia ya kujifunza kwa kina.

Théâtre D'opéra Spatial (kwa Kifaransa, maana yake ni "Ukumbi wa opera wa anga za juu") ni picha ya kwanza ya akili bandia iliyotengenezwa na akili bandia zalishaji ya Midjourney, kushinda tuzo ya sanaa za kidijitali.

Akili bandia zalishi hujifunza alama na miundo ya data za mafunzo kisha hutumia elimu hii kuzalisha data mpya zinazofanana na data za mafunzo.[1]

Marejeo

hariri
  1. "Generative artificial intelligence", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-01-09, iliwekwa mnamo 2024-01-11
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Akili bandia ya kuzalisha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.