Alexander Donald Gwebe Nyirenda


Alexander Donald Gwebe Nyirenda (aliizaliwa Karonga, Malawi [1] 2 Februari 1936 (1936-02-02) (umri 88))[2] ni askari wa Tanzania aliyepata umaarufu kwa kupandisha bendera ya Tanganyika huru juu ya Mlima Kilimanjaro.

Alexander Nyirenda

Stempu yenye Picha Luteni Alexander Nyirenda akipandisha bendera ya Taifa mara baada ya Tanganyika Kupata Uhuru.
Amezaliwa 2 Februari 1936 (1936-02-02) (umri 88)
Karonga, Malawi
Amekufa 2 Desemba 2008 (umri 72)
Saratani ya Umio
Nchi Tanzania
Anafahamika kwa Kwa Kusimiki Mwenge wa Uhuru na Kupandisha bendera ya Taifa Katika kilele cha mlima Kilimanjaro
Kazi yake Mwanajeshi
Mwajiri Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania
Elimu Mchikichini, Malangali, Chuo cha Kifalme cha Kijeshi cha Sandhurst
Mwenza Hilda Simkoko
Watoto 5

Elimu yake hariri

Alisoma katika shule ya msingi ya Mchikichini jijini Dar es Salaam. Alipomaliza elimu ya msingi alichaguliwa kuendelea na masomo ya Upili katika shule ya wavulana ya Malangali iliyoko mkoani Iringa na baadae akaendelea na elimu hiyo Mkoani Tabora na kuhitimu masomo yake mwaka 1957.

Alichaguliwa kuendelea na amali ya kijeshi na mwaka 1958 akachaguliwa kwenda nchini Uingereza katika chuo cha kijeshi kilichoitwa Sandhurst kwa masomo ya uafisa kadeti.

Kazi hariri

Baada ya kumaliza masomo yake alirejea nchini Tanganyika na kujiunga na "Kings African Rifles" mwaka 1960.

Tarehe 9 Desemba mwaka 1962 Nyirenda aliingia kwenye vitabu vya historia kwa kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni na kusimika bendera ya Tanganyika baada ya kupata uhuru kutoka kwa wakoloni na nchi kuwa chini ya Julius Kambarage Nyerere[3].

Aliondoka jeshini Mwezi wa nane mwaka 1964 kama Luteni Kanali.

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  1. https://allafrica.com/stories/201212100036.html
  2. https://eturbonews.com/climb-mount-kilimanjaro-with-a-message-of-hope/
  3. https://madarakanyerere.blogspot.com/2011/12/it-is-third-death-anniversary-today-of.html
  4. https://allafrica.com/stories/201212100036.html