Alibaba Group
Alibaba Group Holding Limited (pia hujulikana kama Alibaba) ni kampuni ya teknolojia ya kimataifa yenye makao makuu yake nchini China iliyobobea katika biashara ya mtandaoni na teknolojia .
Ilianzishwa mnamo 28 Juni 1999 huko Hangzhou,Zhejiang kampuni hiyo hutoa huduma za mauzo ya watumiaji kwa watumiaji (C2C), biashara kwa watumiaji (B2C), na biashara kwa biashara (B2B) kupitia lango za wavuti, pia hutoa huduma za malipo ya kielektroniki, injini za utaftaji wa ununuzi, na huduma za kompyuta ya wingu. Inamiliki na kuendesha matawi mengi ya kampuni ulimwenguni kote katika sekta nyingi za biashara. [1]
Mnamo 19 Septemba 2014, uwekezaji wa shea wa Alibaba (IPO) kwenye Soko la hisa la New York ulikusanya dola za Kimarekani bilioni 25, na kuipa kampuni hiyo thamani ya soko la dola za Kimarekani bilioni 231. Hadi sasa IPO ni kubwa zaidi katika historia duniani.[2] Ni mojawapo ya mashirika 10 yenye thamani zaidi[3] na imetajwa kuwa kampuni ya 31 kwa ukubwa duniani kwenye orodha ya Forbes Global 2000 mwaka 2020.[4] Mnamo Januari 2018, Alibaba ilikuwa kampuni ya pili katika bara la Asia kwa kuwa na thamani ya dola Kimarekani bilioni 500, baada ya mshindani wake kampuni ya Tencent.[5]
Marejeo
hariri- ↑ McClay, Rebecca (25 Julai 2017). "10 Companies Owned by Alibaba". Investopedia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Machi 2019. Iliwekwa mnamo 3 Desemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Alibaba surges 38 percent on massive demand in market debut", Reuters, 19 September 2014.
- ↑ "Beijing's battle to control its homegrown tech giants", Today, 24 September 2017.
- ↑ Murphy, Andrea (13 Mei 2020). "Global 2000". Forbes. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Desemba 2012. Iliwekwa mnamo 27 Agosti 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ JAO, NICOLE. "Alibaba market value hits the $500 billion valuation mark", TechNode, 25 January 2018.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alibaba Group kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |