Alicia Keys
Muimbaji na mwigizaji wa Kimarekani
Alicia Keys (alizaliwa tarehe 25 Januari 1981) ni mwandishi, mtunzi, mwimbaji na mtayarishaji wa muziki wa Marekani.
Alicia Keys | |
---|---|
Alicia Keys, mnamo 2019
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Alicia Augello Cook |
Amezaliwa | 25 Januari 1981 |
Aina ya muziki | Pop |
Kazi yake | Mwanamuziki, mwimbaji |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 1993 - hadi leo |
Studio | RCA Records |
Tovuti | aliciakeys.com |
Alianza kazi ya muziki alipokuwa na umri wa miaka 15 aliposaini mkataba katika lebo ya Columbia Records. Mwaka 2001 alitoa albamu iliyoitwa Songs in A Minor iliyosimamiwa na studio inayoitwa J Records na alifanikiwa kuuza zaidi ya milioni 12 ya nyimbo zake Dunia nzima. Mwaka 2004 alitoa albamu yake ya pili iliyoitwa The Diary of Alicia Keys na kufanikiwa kuwa msanii wa kwanza wa kike kuchukua tuzo ya MTV.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alicia Keys kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |