Mkataba
Mkataba (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: "contract") ni makubaliano ambayo yana nguvu za kisheria, hivyo yanaweza yakadaiwa yatekelezwe. Kumbe si kila mara hivyo kwa ahadi, kwa mfano ile inayotolewa na mzazi kwa mtoto wake.
Sheria zinazoshinikiza utelezaji wa ahadi zinatofautiana kadiri ya nchi, desturi n.k. lakini kwa kawaida inategemea kama waliokubaliana walitaka maneno yao yawe ya kudaiwa hata mbele ya mahakama au serikali.
Mara nyingi, mkataba wenye nguvu ya kisheria huwa kwa maandishi na saini, lakini si lazima iwe hivyo daima.
Upande mmoja ukivunja mkataba, upande wa pili unaweza kufungua kesi.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkataba kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |