Almaty (Kikazakhi: Алматы/- Almaty ; hadi 1994 Alma-Ata) ni mji mkubwa wa Kazakhstan na kitovu chake cha uchumi, elimu na utamaduni. Idadi ya wakazi ni milioni 2. Ilikuwa mji mkuu wa nchi hadi 1996 lakini tangu 1997 serikali ilihamia Astana.

Sehemu ya Mji wa Almaty


Astana na Almaty nchini Kazakhstan

Historia

hariri

Eneo la mji lilikaliwa na watu tangu milenia kabla ya Kristo.

Tangu karne ya 10 BK lilikua hapa mji wa Almatu. Jina lake limepatikana kutokana na sarafu ya Dirham ya mwaka 684 BH (1285 BK). Mji ulistawi kutokana na biashara kwenye barabara ya hariri hadi kuharibiwa kwa biashara hii katika karne ya 14.

Mwaka wanajeshi Warusi walijenga boma karibu na maghofu ya Almatu wakati Urusi ulipoeneza himaya yake katika Asia ya Kati. Mji mpya ulianzishwa kwa jina Verny ((Верный)) ukaitwa hivyo hadi 1921. Baada ya mapinduzi wa kibolsheviki jina likabadilishwa kuwa Alma-Ata. Mji ukawa mji mkuu wa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikazakh ndani ya Umoja wa Kisovyeti.

Tangu 1991 Alma-Ata ilikuwa mji mkuu wa nchi huru mpya Kazakhstan ikabadilishwa jina kuwa Almaty. Serikali iliamua kuhamisha makao makuu ya serikali kwenda katika kitovu cha kijiografia ya nchi na tangu 1997 Almaty si mji mkuu tena.

Lakini makampuni makubwa, vyuo na taasisi za utamaduni vimebaki Almaty.