Angelique Kidjo

Mwanamuziki mashuhuri, muigizaji, na mfanyakazi

Angélique Kidjo (amezaliwa tar. 14 Julai mwaka 1960 nchini Benin) ni mshindi mara tano wa tuzo ya Grammy kama mtunzi na mwimbaji bora. Kidjo anafahamika sana kwa mtindo wake wa kuchanganya miondoko mbali ya kimuziki, pia kuwa mbunifu mzuri wa sini za video.

Angélique Kidjo

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Angélique Kidjo
Amezaliwa 14 Julai 1960 (1960-07-14) (umri 64)Ouidah, Benin
Aina ya muziki Afropop, Afrobeat, reggae, muziki wa dunia, worldbeat, jazz, muziki wa injili, Latin
Kazi yake Mwimbaji
Mtunzi
Miaka ya kazi 1982–hadi leo
Studio Island, Mango, PolyGram, Columbia, Razor & Tie
Tovuti www.kidjo.com

Shughuli za kimuziki

hariri

Kidjo alizaliwa mjini Ouidah, Benin. Wakati kidjo ana umri wa miaka sita alikuwa akijushughulisha na kikundi cha kibisa kilichokuwa kinamilikiwa na mama yake mzazi, mama yake akawa anampa kipaumbele sana katika muziki na kucheza pia. Kuendelea kwa machafuko ya kisiasa nchini Benin kulimpelekea Kidjo kukimbilia Paris Ufaransa mnamo miaka ya 1982.

Alianza kama mwimbaji wa bendi za vichochoroni kabla ya kuanzisha bendi yake mwenyewe, na mwishoni mwa miaka ya 1980 akawa moja kati waimbaji maarufu wa jukwaani huko mjini Paris Ufaransa. Kidjo ameolewa na mwanamuziki pia mtaarishaji aitwae Jean Hebrail kwa pamoja wamezaa mtoto mmoja aitwae Naïma (alizaliwa 1993), na Kidjo kwa sasa anaishi mjini New York, Marekani.

Mengineyo ya kujitolea

hariri

Amekuwa balozi wa kujitolea wa UNICEF tangu 2002.

Kidjo ameanzisha mfuko uitwao Batonga (Kwa kiing: Batonga Foundation) ni mfuko ambao unatoa elimu ya juu ya sekondari kwa wasichana kwa lengo la kuwapa mwongozo wa maisha katika kuibadilisha Afrika. Mfuko pia unakubali ufadhili wa wanafunzi, kujenga shule za sekondari, kuongeza uhandikishaji zaidi, kuboresha viwango vya ufundishaji, kukimu uenezaji wa shule, kusaidia mipango endelevu katika elimu, kutafuta njia ya mbadala ya elimu na kiuwakilisha katika jumuiya kuwa kama ndio kutambua thamani ya elimu kwa wasichana.

Albamu alizotoa

hariri
  • Pretty (Ilitolewa Afrika tu)
  • Parakou (1990)
  • Logozo (1991)
  • Ayé (1994)
  • Fifa (1996)
  • Oremi (1998)
  • Keep : Mchanganyiko wa nyimbo za Angelique Kidjo (2001)
  • Black Ivory Soul (2002)
  • Oyaya] (2004)
  • Djin Djin (2007)

Kidjo pia aliwahi urekodi nyimbo nyingi tu kwa ajili ya filamu mbalimbali.

Octave RFI (1992) Prix Afrique en Creation (1992) Danish Music Awards: Mwimbaji bora wa kike (1995) Kora Music Awards: Mwimaji bora kike wa Afrika(1997) Mobo Awards (2002) Grammy uteuzi ukiwemo na nyimbo bora ya Video ya mwaka 1995 na Albamu bora ya Dunia kwa mwaka wa 1999, 2003 na 2005.

Viungo vya Nje

hariri