Korongo (Gruidae)

Ndege wakubwa wa familia Gruidae
(Elekezwa kutoka Anthropoides)
Korongo
Korongo-taji kijivu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Gruiformes (Ndege kama korongo)
Familia: Gruidae (Ndege walio na mnasaba na korongo)
Vigors, 1825
Ngazi za chini

Jenasi 4, spishi 15:

Korongo hawa (pia mana) ni ndege wa familia ya Gruidae wenye domo fupi na jembamba kuliko lile la korongo wa familia ya Ciconiidae. Spishi nyingi hufanya mikogo ya kubembeleza jike wakitoa sauti kubwa. Huugana kwa maishi yao yote. Spishi za nchi za halijoto wastani huhama kila mwaka kabla ya wakati wa baridi. Korongo hawa hupenda kuwa pamoja na huhama kwa makundi makubwa. Hula kila kitu kinachopatikana, kama panya, watambaazi, amfibia au samaki, hata nafaka na matunda madogo. Spishi za korongo zinatokea mabara yote ghairi ya Amerika ya Kusini.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengi

hariri