Reptilia
Reptilia (Watambaachi) | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mamba ni reptilia mkubwa
| ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Oda 4 (au 5) za reptilia hai:
|
Reptilia (kutoka Kilatini "reptilis" mwenye kutambaa; pia: mtambaazi, mtambaachi, mnyama mtambaaji[1]) ni kundi la wanyama wenye damu baridi, ngozi ya magamba badala ya nywele au manyoya wakipumua kwa mapafu. Siku hizi wataalamu hupendelea jina Sauropsida.
Wanazaa kwa njia ya mayai; wengine wanataga mayai na wadogo wanatoka nje bila ngazi ya kiluwiluwi au kwa spishi kadhaa mayai yanaiva ndani ya tumbo la mama na wadogo wanazaliwa hai.
Kibiolojia ni ngeli ya vertebrata. Jina limetokana na maumbile yao maana wanatambaa na tumbo juu ya ardhi; ama kwa miguu mifupi kama mijusi au bila miguu kama nyoka.
Mwainisho
hariri- Ngeli Reptilia (au Kladi Sauropsida)
- Kladi Eureptilia
- Kladi Romeriida
- Nusungeli Anapsida
- Oda Testudines (makobe)
- Nusungeli Diapsida
- Ngeli ya chini Archosauromorpha
- Ngeli ya chini Lepidosauromorpha
- Oda ya juu Lepidosauria
- Oda Rhynchocephalia (tuatara - wanafanana na mijusi lakini ukoo ni tofauti)
- Oda Squamata (nyoka, mijusi na mijusi-nyungunyungu)
- Oda ya juu Lepidosauria
- Nusungeli Anapsida
- Kladi Romeriida
- Kladi Eureptilia
Dinosauria wa kale walikuwa reptilia wakubwa sana walikwisha miaka milioni 65 iliyopita. Kufuatana na vumbuzi za hivi karibuni ndege hufikiriwa kuwa na nasaba na dinosauri (kutoka kwa nusuoda ya Theropoda).
Maelezo
haririPicha
hariri-
Joka wa Komodo ni mjusi mkubwa kabisa
-
Hata ndege ni reptilia!
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Reptilia kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |