Anton Durcovici
Anton Durcovici (17 Mei 1888 – 10 Desemba 1951) alikuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Romania na Askofu wa Iași kuanzia mwaka 1947 hadi kifo chake.
Durcovici alikuwa mwathirika wa utawala wa Kikomunisti wa Romania, ambapo alikamatwa na kufungwa. Alifariki akiwa gerezani kutokana na mateso aliyopitia chini ya utawala huo.[1]
Papa Fransisko alimtangaza mwenye heri tarehe 17 Mei 2014.
Marejeo
hariri- ↑ "Beato Anton Durcovici". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo 4 Machi 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |