Antonio Conte
Antonio Conte (matamshi ya Kiitalia: [anˈtɔːnjo ˈkonte]; amezaliwa 31 Julai 1969) ni meneja wa mpira wa miguu wa Italia na mchezaji wa zamani.
Jinsia | mume |
---|---|
Nchi ya uraia | Italia |
Nchi anayoitumikia | Italia |
Jina katika lugha mama | Antonio Conte |
Jina halisi | Antonio |
Jina la familia | Conte |
Nickname | Conte, Padrino, Martello |
Tarehe ya kuzaliwa | 31 Julai 1969 |
Mahali alipozaliwa | Lecce |
Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihi | Kiitalia |
Kazi | association football player, association football manager |
Mwajiri | Siena FC |
Nafasi anayocheza kwenye timu | Kiungo |
Mwanachama wa timu ya michezo | Juventus F.C., US Lecce, Italy men's national association football team |
Coach of sports team | SSC Napoli |
Mchezo | mpira wa miguu |
Ameshiriki | 1994 FIFA World Cup, UEFA Euro 2000 |
Tuzo iliyopokelewa | Knight of the Order of Merit of the Italian Republic |
Kwa sasa ni kocha mkuu wa klabu ya Internazionale Milano. Alichukua nafasi hiyo akitokea Chelsea ya Uingereza.
Conte anazungumza lugha ya Kiitalia na Kiingereza. Ni Mkristo muumini wa Kanisa Katoliki. Conte na mkewe Elisabetta wana mtoto mmoja wa kike anayefahamika kwa jina la Vittoria. Wawili hao walikuwa katika mahusiano ya miaka 15 kabla ya kuoana mnamo Juni 2013.
Mwaka 2012 Conte alikutwa na kashfa ya kupanga matokeo wakati huo akiwa kocha wa klabu ya Siena ya Italia akiwa na mchezaji mwenzake Filippo Carobbio walihusishwa katika kupanga matokeo kwa kucheza kamari msimu huo wa 2011-12.
Katika kashfa hiyo ilielezwa kuwa mmiliki wa Siena Massimo Mezzaroma alipeleka ujumbe kwa wachezaji akiwataka wahakikishe mchezo wao dhidi ya Novara umalizike kwa sare. Kwa kufanya hivyo Mezzaroma alipata faida kubwa. Conte aliweka bayana namna familia yake ilivyomsaidia hususani mkewe ambaye alitoa msaada mkubwa kwake.
Akiwa mchezaji alikuwa akicheza nafasi ya kiungo. Alianza soka lake katika klabu ya Lecce na baadaye kuwa mchezaji mwenye mvuto na mwenye ushawishi katika klabu ya Juventus. Aliwahi kuwa nahodha wa Juventus katika Ligi ya Mabingwa barani ulaya pia serie A na michuano mingine. Pia alicheza timu ya taifa ya Italia ‘Azzuri’ na kushiriki Kombe la Dunia mwaka 1994 na Mataifa ya Ulaya Euro 2000. Na katika mara zote hizo Italia ilishika nafasi ya pili.
Kazi ya ukocha alianza mwaka 2006 na baadaye kuiongoza klabu ya Bari kutwaa taji la Serie B msimu wa 2008-09. Miaka miwili baadaye aliipandisha Siena katika Serie B. Alikwenda kuinoa Juventus mwaka 2011 alikoweka mfumo 3-5-2 na kufanikiwa kutwaa mataji matatu ya Serie A. Mwaka 2014 aliiongoza timu ya taifa hadi kampeni za Mataifa ya Ulaya mwaka 2016. Alitua katika klabu ya Chelsea Aprili 2016 na katika msimu wa kwanza alitwaa taji la Ligi Kuu ya England (EPL). Baada ya hapo alitwaa taji la FA katika msimu wake wa pili.
Alitimuliwa Julai 2018 kuinoa klabu ya Chelsea na Mei 31, 2019 alitangazwa kocha mpya wa klabu ya Inter Milan.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Antonio Conte kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |