Chelsea F.C.

Chelsea Football Club ni klabu ya mpira wa miguu ya nchini Uingereza iliyo na maskani yake Fulham, London. Klabu hii ilianzishwa mwaka 1905, na kwa miaka mingi sana imekuwa ikishiriki ligi kuu ya Uingereza. Uwanja wao wa nyumbani ni Stamford Bridge ambao una uwezo wa kuingiza watazamaji 41,837, wameutumia uwanja huu tangu klabu ilivyoanzishwa.

Chelsea
Picha:Chelsea FC.svg
Jina kamiliChelsea Football Club
Jina la utaniThe Pensioners, The Blues
ImeanzishwaMachi 10, 1905; miaka 116 iliyopita (1905-03-10)
UwanjaStamford Bridge
(Uwezo: 41,841)
MmilikiRoman Abramovich
MwenyekitiBruce Buck
MenejaThomas Tuchel
LigiPremier League
2017-18Premier League, 3th
Rangi nyumbani
Rangi za safari

Chelsea, kwa mara ya kwanza ilipata mafanikio makubwa mwaka 1955, ambapo walipata ubingwa wa ligi, na walishinda mataji kadhaa katika miaka ya 1960, 1970, 1990 na 2000. Klabu hii imefurahia zaidi mafanikio katika miongo miwili ilopita, kwa kushinda mataji makubwa 15 tangu mwaka 1997.

Nyumbani, Chelsea imeshinda ubingwa wa ligi mara nne, kombe la FA mara saba, kombe la ligi mara nne, pamoja na ngao za jamii mara nne. Na kimataifa Chelsea imeshashinda UEFA Cup Winners' Cups mara mbili, UEFA Super Cup moja, UEFA Europa League moja na UEFA Champions League moja. Chelsea ndio klabu pekee kutoka London kushinda UEFA Champions League, na ni moja kati ya klabu nne kutoka Uingereza, kuchukua makombe yote makubwa matatu ya Ulaya.

Kwa kawaida Chelsea huvaa jezi ya blu, kaptula blu na soksi nyeupe. Nembo ya klabu imebadilishwa mara nyingi kulingana na wakati na kuboresha muonekano wa klabu. Nembo ya sasa inaonesha picha ya simba akiwa amebeba mkuki. Tangu Julai 2003, Chelsea imekuwa ikimilikiwa na Bilionea wa Kirusi, Roman Abramovich.

WachezajiEdit

 
Wachezaji wa Chelsea
As of 7 January 2018.[1]

Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.

Na. Nafasi Mchezaji
1   GK Kepa Arrizabalaga
2   DF Antonio Rüdiger
6   {{{name}}}
3   DF Marcos Alonso
30   DF David Luiz
7   MF N'golo kantè
8   MF Ross Barkley
29   FW Alvaro morata
11   MF Pedro (footballer born 1991)
10   MF Eden Hazard
Na. Nafasi Mchezaji
18   FW O. Giroud
5   MF Jorginho
22   MF Willian
23   GK Mark Schwarzer
24   DF Gary Cahill
26   DF John Terry (captain)
27   DF Nathan Aké
28   DF César Azpilicueta
31   FW Ariri Charles
33   DF Tomáš Kalas
40   GK Henrique Hilário
46   GK Jamal Blackman

TuzoEdit

  • Ligi Kuu (6) 1954-1955, 2004-2005, 2005-2006, 2009-2010, 2011-2012, 2016-2017
  • FA Cup (7) 1970, 1997, 2000, 2007, 2009, 2010, 2018
  • Kombe la Ligi (4) 1965, 1998, 2005, 2007;
  • Ngao ya Jamii (4) 1955, 2000,2005, 2009
  • UEFA Cup Winners' Cup (2) 1971, 1998
  • UEFA Super Cup (1) 1998, 1999, 2003
  • Full Members Cup (2) 1986, 1990
  • FA Youth-cup (3) 1960, 1961, 2010

TanbihiEdit

  1. First Team Squad List. Chelsea F.C. Iliwekwa mnamo 7 August 2018.