Lukungu

(Elekezwa kutoka Apaloderma)
Lukungu
Lukungu wa kawaida
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Trogoniformes (Ndege kama lukungu)
Familia: Trogonidae (Ndege walio na mnasaba na lukungu)
Jenasi: Apalharpactes

Apaloderma Swainson, 1833
Euptilotis Gould, 1858
Harpactes Swainson, 1833
Pharomachrus De la Llave, 1832
Priotelus G.R. Gray, 1840
Trogon Brisson, 1760

Lukungu ni ndege wa familia Trogonidae. Wanatokea misituni kwa tropiki katika Afrika, Asia na Amerika. Ndege hawa wana ukubwa wa kwenzi mkubwa. Rangi zao ni kali na spishi za Afrika zina tumbo jekundu na mgongo kijani. Hula wadudu hasa lakini spishi za Amerika na Asia hula matunda pia. Dumu au dumu na jike pamoja huchimba tundu katika mti unaooza au kichuguu ili kutaga mayai ndani yake. “Violaceous trogon” hutengeneza tago lake mara nyingi ndani ya tundu la nyigu. Jike huyataga mayai 2-4. Makinda huota manyoya haraka sana: katika wiki mbili hadi tatu, pengine wiki nne.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri