Apokrifa (kutoka neno la Kigiriki ἀπόκρυφος, apókruphos, yaani "iliyofichika") ni jina linalotumika katika Ukristo kuanzia karne ya 5 kutajia vitabu ambavyo madhehebu husika hayavikubali katika Biblia.

Hivyo vitabu vilevile vinaweza kuwa vitakatifu kwa madhehebu kadhaa lakini si kwa mengine.

Lakini kuna vitabu vingine ambavyo vinatazamwa na Wakristo wote kuwa ni apokrifa, kwa mfano "Maisha ya Adamu na Eva".

Maelezo ya undani zaidi yanapatikana katika makala Deuterokanoni kuhusu vitabu maarufu zaidi vinavyokubaliwa na Kanisa Katoliki na wengineo kama Neno la Mungu, lakini si na Waprotestanti wengi.

Marejeo

hariri

Vitabu vyenyewe

Ufafanuzi

  • O. F. Fritzsche and Grimm, Kurzgef. exeget. Handbuch zu den Apok. des A.T. (Leipzig, 1851–1860)
  • Edwin Cone Bissell, Apocrypha of the Old Testament (Edinburgh, 1880)
  • Otto Zöckler, Die Apokryphen des Alten Testaments (Munchen, 1891)
  • Henry Wace, The Apocrypha ("Speaker's Commentary") (1888)

Utangulizi

Viungo vya nje

hariri