Biblia
Biblia ni jina la jumla kwa ajili ya vitabu vitakatifu vya dini ya Uyahudi na hasa ya Ukristo.

Neno limetokana na lugha ya Kigiriki ambayo ndani yake βιβλία (biblia) ina maana ya "vitabu" ikiwa ni wingi wa βιβλος (biblos). Hii ni kwa sababu Biblia ni mkusanyo wa maandiko mbalimbali yaliyoweza kutungwa kwa muda wa miaka 1000 hivi.
Hivyo Biblia ni tofauti na vitabu vingine kwa sababu iliandikwa na watu mbalimbali ambao hawakuwa pamoja wala hawakuandika kwa wakati mmoja, lakini vitabu vyote vimekusanywa na kuunda kitabu kimoja cha Biblia. Inasadikiwa na Wayahudi na Wakristo kwamba "Biblia ni kitabu kilichoandikwa na watu kwa uwezo wa Mungu".
Tunaweza kutofautisha:
- Biblia ya Kiebrania au Tanakh inavyotumiwa na Wayahudi. Vitabu hivyo 39 kwa Kanisa Katoliki na wengineo ni sehemu kuu ya vile 46 vinavyoitwa "Agano la Kale" (wakati Wakristo wengine, hasa Waprotestanti, wanakubali hivyo 39 tu). Ndilo sehemu ya kwanza ya
- Biblia ya Kikristo inavyotumiwa na Wakristo yenye vitabu vya Agano la Kale pamoja na Agano Jipya.
Viungo vya nje
- Biblia ya Kiswahili Union version
- Toleo la Kiswahili la Biblica Translation 2006
- Agano Jipya pekee (tafsiri kwa Kiswahili chepesi)
- Biblia
Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDKYudithiDKEsta Wamakabayo IDKWamakabayo IIDKYobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DKSiraDKWimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDKEzekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.