Neno la Mungu ni namna ambayo wafuasi wa dini kadhaa wanavyotazama misahafu yao ili kusisitiza imani yao ya kuwa hiyo iliandikwa kadiri ya Mungu na kuleta kwa usahihi ufunuo wake.

Kwa namna ya pekee Uyahudi na Ukristo vinaita hivyo Biblia.

Zaidi ya hayo, katika Agano Jipya Mtume Yohane anamwita hivyo Yesu Kristo ili kueleza asili yake ya Kimungu kabla ya kuzaliwa binadamu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kutokana na Bikira Maria.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.