Ariel Wayz
msanii wa Rwanda
Ariel Wayz (alizaliwa Rubavu, Jimbo la Magharibi) ni msanii wa Rwanda.
Mtoto wa tano katika familia ya watoto nane, amerithi kuwa mwanamuziki kwa sababu mama yake alikuwa akiimba katika orchester Inngeri miaka ya 1990.
Ariel alilenga tu kufuata muziki kama taaluma na alijua Shule ya muziki ya Nyundo ingemsaidia kutimiza ndoto yake.
Alipokuwa akikua, alikuwa na macho ya kuwa mwanamuziki mkubwa siku moja kwa hivyo mwanadada huyo hakufikiria mara mbili na akachangamkia fursa wakati shule ya muziki ya Nyundo ilipofanya majaribio ya kutafuta talanta mpya ya muziki ya kuinua mwaka wa 2015.
Mwaka uliofuata, shule ilimpa ufadhili wa kusoma muziki na kumpa jukwaa la kugundua talanta aliyonayo kimuziki.[1]
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ariel Wayz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |