Article One
Article One ni bendi ya Kikristo kutoka Kanada hasa London, Ontario. Bendi lenyewe linahusu:
- Nathan Piche(mwimbaji,mchezaji gitaa)
- Matt Piche(mwimbaji)
- Dave DeSmit(mchezaji ngoma)
- Nolan Verner(mchezaji gitaa)
Echoing Angels | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Aina ya muziki | Nyimbo za kisasa za Kikristo |
Kazi yake | Wanamuziki |
Ala | Gitaa |
Miaka ya kazi | 2003 hadi sasa |
Studio | INO Records,EMI Japan |
Tovuti | www.articleonemusic.com |
Wanachama wa sasa | |
Nathan Piche Matt Piche Dave DeSmit Nolan Verner | |
Wanachama wa zamani | |
Mark Laidman |
Historia
haririNathan na Matt Piche walikuwa wamelelewa katika familia ya wanamuziki. Wazazi wao walikuwa walimu wa muziki na dada yao alikuwa gwiji wa kucheza gitaa.[1] Baba yao alikuwa mwanamuziki wa Kikristo ambaye alizuru nchi nzima kama msanii pekee yake,yaani bila bendi. Matt alianza kucheza ala ya muziki akiwa umri wa miaka mitano na Nathan akaanza mwaka mmoja baadaye. Masomo ya muziki kwa Dave DeSmit's yalianza katika shule ya msingi.[1] Matt started playing violin when he was five years old and Nathan started playing piano a year later.[1]
Jina
haririHapo awali walijiita Appertain Display[2]. Baadaye,bendi lilichukua jina lake la sasa kutoka makala ya kwanza ya Azimio la Haki za Binadamu yaliyoonyeshwa na bendi la U2 katika ziara yao ya Vertigo. [3]Makala hayo yanasema "Wanadamu wote wamezaliwa huru na sawa katika heshima na haki.Wamejaliwa na akili dhamiri na nafsi,na wanastahili kutendeana vitendo kwa roho ya undugu."
Diskografia
haririAlbamu
haririHapo tarehe 8 Mei 2007,walitoa albamu yao ya studio kwa kupitia studio ya Inpop Records Albamu yao ya pili ilitolewa tarehe 27 Mei 2008. Toleo spesheli la albamu yao ya pili lilitolewa Ujapani lilikuwa na wimbo unaoitwa In no time at all kutoka albmau yao ya kwanza ukiwa wimbo wa kuongezwa katika albamu hiyo.[2]
Mwaka | Jina la albamu | Studio |
---|---|---|
2003 | Appertain Display EP | Wakijitegemea |
2003 | Appertain Display | Wakijitegemea |
2006 | AO | Wakijitegemea |
2007 | AO | Inpop Records |
2008 | Colors and Sounds | Inpop Records |
2008 | Colors and Sounds (Japanese Special Edition) | EMI Japan |
Nyimbo Zao
haririWimbo waoWithout You I'm Not Alright ulifika # 8 katika chati ya nyimbo za kisasa za Kikristo nchini Marekani (Juni 2008). Taken By The Storm uliingia katika nyimbo bora kumi katika chati ya chati ya nyimbo za kisasa za Kikristo nchini Marekani.[4] "Taken By The Storm" climbed into the Top 10 on the U.S. Contemporary Christian Music chart.[5]
Mwaka | Jina la Wimbo | Albamu |
---|---|---|
2008 | Without You (I'm Not Alright) | Colors and Sounds |
2008 | Taken By the Storm | Colors and Sounds |
Nyimbo katika albamu za kompilesheni
hariri- Launch: Inferno, "Slow Down" (CMC, 2007)
- YourMusicZone.com #1s, "Say It Again" (CMC, 2007)
- Canada Rocks, "Without You (I'm Not Alright)" (CMC, 2008)
- Sea to Sea: Christmas, "One Gift" (Lakeside, 2009)
Tuzo
hariri- 2006 washindani katika tuzo ya Wanamuziki wapya wa mwaka.
- 2008 Albamu ya Nyimbo za Kisasa za Kikristo kwa albamu yao ya: Colors and Sounds
- 2008 washindani, Wimbo wa Kisasa wa mwaka: Without You (I’m Not Alright)
- Washindani wa tuzo ya Juno 2009, Albamu ya nyimbo za kisasa za Kikristo: Colors and Sounds
Ziara
haririReign In Us (Marekani na Kanada) pamoja na Starfield 2009
Rock What You Got (Marekani) wakiwa pamoja na Superchick na Stellar Kart - 2008
Newsboys GO Marekani) - 2008
Shoutfest (Marekani) - 2007
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 Article One Biography; Christian Music Central; Retrieved 2008-04-08
- ↑ 2.0 2.1 Article One Biography; Jesus Freak Hideout; Retrieved 2008-04-08
- ↑ Music review of Article One; Russ Breimeier; Mei 2007; Christianity Today; Retrieved 2008-04-08
- ↑ Contemporary Christian Music Chart for R&R magazine as reported at the Weekend 22; 5 Aprili 2008; Retrieved 2008-04-05
- ↑ [1] Archived 14 Oktoba 2008 at the Wayback Machine. R&R magazine; Retrieved 2008-01-14
Viungo vya nje
hariri- Tovuti Rasmi Archived 28 Januari 2010 at the Wayback Machine.
- Article One katika MySpace