Ashoka
Ashoka (pia: Asoka) alikuwa mtawala wa Uhindi kati ya 273 KK na 232 KK. Alizaliwa katika nasaba ya Maurya akafaulu kupanua himaya yake juu ya maeneo ya nchi za kisasa za Uhindi, Pakistan, Bangladesh na Sri Lanka.
Mara nyingi anatajwa kama mtawala mkuu katika historia ya Bara Hindi. Baada ya vita aliyoshinda mnamo 265/263 KK alishtuka juu ya vifo vingi na uharibifu akageuka kuwa Mbuddha. Mnamo mwaka 260 KK alitangaza Ubuddha kuwa dini rasmi ya milki yake akatuma wamisionari kutangaza imani hiyo katika nchi jirani.
Hakupiga vita tena lakini alitumia nguvu yake kujenga maendeleo ya milki yake. Anakumbukwa hasa kutokana na matangazo yake yaliyochongwa kwenye mawe ya majengo katika sehemu mbalimbali za milki yake kama vile: "Wanadamu wote ni watoto wangu. Mimi ni kama baba yao. Jinsi kila baba anavyotaka mema na heri kwa watoto wake nami ninataka watu wote wawe na raha siku zote".
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ashoka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |