Adamu (kwa Kiebrania: אָדָם maana yake mtu, mtu wa udongo, chaudongo, au wa udongo mwekundu) ni jina analopewa mtu wa kwanza katika Biblia. Anatajwa na Kurani pia.

Uumbaji wa Adamu ulivyochorwa (1511) na Michelangelo Buonarroti katika Cappella Sistina, huko Vatikano. Ni mmojawapo kati ya michoro maarufu zaidi duniani.
Uuumbaji wa Adamu kadiri ya Andrea Pisano, 1334-1336

Kadiri ya kitabu cha Mwanzo, alizaliana na mke wake Eva watu wote waliopo duniani, ambao kwa sababu hiyo wanaitwa binadamu; kwa namna ya pekee waliweza kuzaa wenyewe Kaini, Abeli na Seti.

Kanisa Katoliki linamheshimu kama mtakatifu kila tarehe 24 Desemba[1].

Katika Biblia hariri

 
Heinrich Aldegrever, Adamu na simba, wakiishi kwa amani kabla ya Dhambi ya Asili
 
Eva akiumbwa kwa ubavu wa Adamu alivyochongwa na (Lorenzo Maitani na shule yake, upande wa mbele wa Kanisa kuu la Orvieto).

Uumbaji wa watu wa kwanza unasimuliwa na kitabu cha Mwanzo mara mbili: katika 1,26-28 na katika 2,7-22.

Masimulizi hayo yanayotofautiana katika vipengele mbalimbali hayadai yachukuliwe kama habari za historia zinazoandikwa siku hizi. Yanatokana na tafakuri ya kina juu ya hali ya binadamu kwa lengo la kuelewa asili yake.

Katika Kurani hariri

Humo Adamu anatajwa kwa namna inayofanana na ile ya Biblia. Anahesabiwa kuwa mtume wa kwanza.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Adamu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.