Ato Malinda
Ato Malinda ni miongoni mwa wasanii wa kike wachache wa maonyesho ya Afrika Mashariki na anapambana ili sanaa hiyo ipate kukubalika. Alizaliwa Kenya mnamo 1981, akiwa mtoto wa mama kutoka Kenya na baba kutoka Uganda. Alikuwa anaishi Uholanzi na baadae alirejea Kenya.
Ato Malinda | |
---|---|
| |
Jina la kuzaliwa | Ato Malinda |
Nchi | Kenya |
Elimu
haririBaada ya kuhitimu Shule ya upili (sekondari) alikwenda Marekani kusomea historia ya sanaa na biolojia ya molekuli katika chuo kikuu cha Texas. Alikuwa na ukuaji mgumu udogoni kwa kushindwa kutimiza matamanio ya baba yake ya kuwa daktari, pamoja na kukabiliana na aibu ya kuwa msagaji katika jamii yake.
Mwaka 2006, baada ya kuhamia Uingereza kwa muda, alipata tena hamasa ya kuendelea na sanaa.[1] Hurejea nchini Kenya mara kwa mara ambapo huwa anafanya kazi katika tasnia mbalimbali za sanaa: sanaa ya video, sanaa ya maonyesho, uchoraji na kupaka rangi.
Ato Malinda awali alifahamika kama Alex Mawimbi. Jina hili lilikuja kusimama zaidi kama kumbukumbu ya baba yake mdhalilishaji wa familia. Baada ya kifo cha mama mkwe wake, aliamua kutotumia tena jina hilo. Alex kwa upande wa pili ni jina zuri linaloelezea mawimbi kwa Kiswahili - Ishara ya Bahari ya Hindi inayokapakana na Kenya, nchi iliyopo katika kitambulisho chake.[2]
Marejeo
hariri- ↑ Radar, Art. "Ato Malinda on sexuality, African feminism and performance as art – interview | Art Radar" (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-19. Iliwekwa mnamo 2020-08-20.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help) - ↑ Bouwhuis, Jelle (2019-02-02). "Alex Mawimbi". AFRICANAH.ORG (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-08-20.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ato Malinda kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |