Ayub Ogada

mwimbaji wa Kenya

Job Seda (1956 - 1 Februari 2019), [1] anayejulikana zaidi kama Ayub Ogada, alikuwa mwimbaji wa chini Kenya. Alikuwa mwimbaji aliyependelea nyatiti (kinubi chenye nyuzi nane ambacho asili yake ni ya Wajaluo, kabila la Nyanza Kenya) kama chombo chake cha sifa. Muziki wake unajulikana kuwa na hisia za kiasili , kuwa na nyimbo za ndege, miito ya wanyama na sauti za watoto wanaocheza. 

Job Seda
Amezaliwa 1959
Mombasa,Kenya
Amekufa 1 Februari 2019
Nchi Kenya
Majina mengine Ayub Ogada
Kazi yake Mwimbaji

Wasifu

hariri

Ayub Ogada alizaliwa mwaka 1956 huko Mombasa, Kenya. Yeye ni mzao wa Wajaluo wa Nyanza Kenya na alishawishiwa na urithi wao wa muziki na wazazi wake ambao walikuwa wanamuziki. Walitumbuiza muziki wa Kiluo kwa watazamaji wa Kenya na Marekani. Uzoefu wa Ayub wa kusafiri na wazazi wake hadi Marekani ulimfanya kujua tamaduni za magharibi na za Kiafrika zilikua na ushawishi kubwa kwenye muziki na mtazamo wake. [2]

Marejeo

hariri
  1. Victor Otieno. "Legendary musician Ayub Ogada dies at 63". Nation.co.ke. Iliwekwa mnamo 2020-04-23.
  2. "Biography". Ayubogada.com.
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ayub Ogada kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.