Babeldaob

(Elekezwa kutoka Babelthuap)

Babeldaob (pia Babelthuap) ni kisiwa kikubwa cha nchi ya visiwani ya Palau. Eneo lake ni km² 331 au asilimia 70 ya eneo lote la taifa.

Kisiwa cha Babeldaob / Babelthuap kwenye kaskazini ya Palau

Kisiwani kuna mji mkuu wa Melekeok na mikoa tisa kati ya 16 ya Palau.

Maadam visiwa vingine vya Palau ni tambarare kabisa, Babeldoab kuna mlima Ngerchelchuus wenye kimo cha mita 242.

Kwenye mkoa wa Airai upande wa kusini upo uwanja wa ndege wa kimataifa.