Baby Madaha

Mwigizaji na mwanamuziki wa Tanzania

Baby Madaha (alizaliwa jijini Mwanza 19 Novemba 1988) ni mwanamke aliyejikita katika tasnia ya filamu za Kitanzania pamoja na muziki. Mwanadada huyu alijishindia tuzo maarufu nchini Tanzania ya BSS- Bongo Star Search mwaka 2007.Baby Madaha ametamba zaidi na kibao chake cha Amore[1].

Baby Madaha
AmezaliwaBaby Joseph Madaha
19 Novemba 1988 (1988-11-19) (umri 35)
UtaifaMtanzania
Kazi yakeMuigizaji, msanii wa muziki wa kizazi kipya,
Miaka ya kazi2000-hadi sasa

Mwaka 2013 alisaini mkataba na lebo ya muziki nchini Kenya iitwayo Candy n Candy[2].

Katika tasnia ya filamu amejulikana sana kwa filamu iitwayo Nani ambayo ilimpatia tuzo huko Ujerumani.

Baadhi ya tamthilia alizowahi kucheza ni

  • Blessed by God
  • Tifu la mwaka [3]
  • Misukosuko
  • Ray of hope


Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-13. Iliwekwa mnamo 2019-07-20. 
  2. https://www.the-star.co.ke/news/2013/09/14/candy-n-candy-records-signs-another-bongo-artiste_c830495
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-29. Iliwekwa mnamo 2018-12-01. 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Baby Madaha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Baby Madaha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.