Bafu za Hamamni, Zanzibar

Majengo ya Tanzania
(Elekezwa kutoka Bafu za Hamami, Zanzibar)

Bafu za Kiajemi za Hamamni zipo katika jengo la kihistoria la Mji Mkongwe Zanzibar. Jina Hamamni pia linatumika kutaja ujirani ambapo jengo hilo lipo.

Muonekano wa Bafu za Kiajemi za Hamamni, Juni 2019
Mlango wa kuingilia

Historia

hariri

Jengo lilijengwa kwenye mwaka usiorekodiwa kwa amri ya Sultani Barghash bin Said aliyetawala kati ya 1870 na 1888. Kusudi lake lilikuwa bafu kwa umma. Bafu ya aina hiyo huitwa “hamam” (حمام) kwa Kiarabu na neno hilo liliingia pia katika Kiswahili kwa umbo la “hamami” au “hamamu”. Jina “Hamamni”[1] inamaanishe “kwenye hamam”. Ilhali kulikuwa na kiingilio watu maskini hawakuweza kuitumia[2].

Mbunifu alikuwa Haji Gulam Hussein mwenye asili ya Uajemi (Iran)[3]. Jengo lilitumiwa hadi likutumiwa kwa shughuli hii hadi 1920.

Muundo wa Bafu za Hamamni

hariri

Jengo lina vyumba kadhaa mbeleni ambako watu waliweza kuvua nguo na kupata huduma ya kinyozi. Kutoka hapa waliendelea hadi sehemu ya joto, ambako moto chini ya chumba kilisababisha halijoto ya juu na wateja walikaa hapa hadi walitoa jasho. Sasa waliweza kuendelea katika vyumba vya bafu ya maji moto au baridi, pamoja na kuingia katika ukumbi mwenye beseni kubwa yenye pembe sita. Kando yake yalikuwa vyumba vidogo vya huduma ya kunyoa nywele za mwilini kufuatana na desturi ya Kiislamu na vyoo.

Kiasili kulikuwa pia na mgahawa lakini sehemu hiyo ilibadilishwa baadaye kuwa makazi binafsi[4]. Bafu zilifunguliwa kwenye nyakati tofauti kwa wanaume na wanawake.

Bafu hazifanyi kazi tena, lakini zineweza kutembelewa na wageni na ni vivutio vya utalii wa Mji Mkongwe[5].

Marejeo

hariri
  1. Matamshi sahihi zaidi itakuwa ni hamaam-ni, kutokana na neno la kiasili
  2. Ling. The Hamamni Persian Baths, tovuti ya Zanzibar.cc
  3. Linganisha Hamamni Baths, Archnet.org
  4. ling. Hamamni Baths, tovuti ya archnet.org
  5. ling. Bradt Travel Guide

Vyanzo

hariri
  • Zanzibar Big Hamamni, tovuti ya Zamaniproject. org, ya Chuo Kikuu cha Cape Town, inayoonyesha mahali pa kumbukumbu pa Afrika
  • Hamamni Baths, tovuti ya archnet.org inayotunzwa na taasisi ya Aga Khan;
  • The Hamamni Persian Baths, tovuti binafsi ya Zanzibar.cc kuhusu utamaduni, historia na utalii wa Zanzibar, imeangaliwa kupitia archive.org, hali ya mwaka 2015
  • The Hamamni Baths, tovuti ya Zanzibar Travel Guide yenye matini kutoka Bradt Travel Guide Zanzibar