Baharia Sindbad
Baharia Sindbad (pia: Sinbad; Kar. السندباد البحري as-Sindibād al-baḥri; Kaj.: سندباد Sandbād) ni jina la baharia na mshujaa wa hadithi kadhaa katika mkusanyiko wa fasihi ya Kiarabu unaopatikana katika kitabu cha Alfu Lela U Lela (Usiku Elfu na Moja). Katika hadithi hizi Sindbad ni mtu wa mji wa Basra (Iraki ya leo) wakati wa Ukhalifa wa Waabbasi na hasa khalifa Harun al-Rashid.
Hadithi ya Sindbad zinasimulia habari za safari zake saba kwenye bahari upande wa mashariki wa Afrika na kusini za Asia. Katika safari hizi anakutana na maajabu mengi, madubwana na kupita kwenye hatari nyingi.