Bamba
Bamba ni kata ya kaunti ya Kilifi, eneo bunge la Ganze, nchini Kenya[1].
Eneo hilo lilifanywa maarufu na wimbo wa kiasilia, 'Safari ya Bamba ni Machero', uliotungwa wa mwalimu Stephen Ngumbau, mkufunzi wa somo la muziki katika chuo cha mafunzo ya waalimu cha Ribe kilichoko katika kaunti ya Kilifi, pwani mwa Kenya. Wimbo huo ulikuwa unawashauri wasafiri wanaolekea Bamba kuwa eneo hilo liko mbali na wangehitajika kuamka macheo ili wafike kwa wakati. Japo kwa sasa Bamba ni mji unaokua na kuna barabara mpya ya lami inayounganisha eneo hilo na mji mdogo wa Miritini, Kaunti ya Mombasa kwa haraka.
Tanbihi
hariri- ↑ Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency Archived Septemba 29, 2007, at the Wayback Machine
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bamba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |