Kaunti ya Kilifi ni kaunti nchini Kenya katika eneo la Mkoa wa Pwani wa awali. Ilianzishwa mwaka 2010 kwa kuunganisha wilaya za Kilifi na Malindi.

Kaunti ya Kilifi
Kaunti
Bendera Nembo ya Serikali
Kilifi County in Kenya.svg
Kaunti ya Kilifi katika Kenya
Nchi Kenya
Namba3
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Pwani
Makao MakuuKilifi
Miji mingineMalindi
GavanaAmason Jefa Kingi
Naibu wa GavanaGideon Edmund Saburi
SenetaStewart Mwachiru Shadrach Madzayo
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Getrude Mbeyu Mwanyanje
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Kilifi
SpikaJimmy Kahindi
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa35
Maeneo bunge/Kaunti ndogo7
Eneokm2 12 539.7 (sq mi 4 841.6)
Idadi ya watu1,453,787
Wiani wa idadi ya watu116
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutikilifi.go.ke

Eneo lake ni km² 12,539.7. Eneo hilo lilikuwa na wakazi 1,453,787 wakati wa sensa ya mwaka 2019, msongamano ukiwa hivyo wa watu 116 kwa kilometa mraba[1].

Mji mkuu uko Kilifi lakini mji mkubwa zaidi ni Malindi.

Kiongozi wa serikali yake ni gavana anayechaguliwa na wananchi.

Eneo la kaunti liko upande wa kaskazini na kaskazini-mashariki ya Mombasa. Sehemu zinazotembelewa na watalii ni hasa Kikambala, Watamu, Malindi na Kilifi.

Utawala

hariri

Kilifi huwa na majimbo ya uchaguzi wa bunge 7 pamoja na kumchagua seneta mmoja na mbunge mmoja wa viti maalum vya wanawake. Kaunti ya Kilifi ina maeneo bunge yafuatayo[2]:

Eneo bunge Idadi ya kata Kata
Kilifi Kaskazini 7 Tezo, Sokoni, Kibarani, Dabaso, Matsangoni, Watamu, Mnarani.
Kilifi Kusini 5 Junju, Mwarakaya, Shimo la Tewa, Chasimba, Mtepeni
Kaloleni 4 Mariakani, Kayafungo, Kaloleni, Mwanamwinga
Rabai 4 Mwawesa, Ruruma, Kambe-Ribe, Rabai/Kisurutuni
Ganze 4 Ganze, Bamba, Jaribuni, Sokoke
Malindi 5 Jilore, Kakuyuni, Ganda, Malindi Mjini, Shella
Magarini 6 Maarafa, Magarini, Gongoni, Adu, Garashi, Sabaki
35

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3]

hariri
  • Chonyi 62,335
  • Ganze 143,906
  • Kaloleni 193,682
  • Kauma 22,638
  • Kilifi North 178,824
  • Kilifi South 206,753
  • Magarini 191,610
  • Malindi 333,226
  • Rabai 120,813

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya Nje

hariri

3°40′00″S 39°45′00″E / 3.66667°S 39.75°E / -3.66667; 39.75