Bamba la Amerika ya Kusini

Bamba la Amerika ya Kusini ni moja ya mabamba ya gandunia ya dunia yetu. Lipo chini ya bara la Amerika ya Kusini na chini ya sehemu kubwa za bahari Atlantiki zinazopakana nalo yaani tako la bara. Ni kati ya mabamba makubwa zaidi duniani.

Bamba la Amerika ya Kusini (rangi ya zambarau) kati ya mabamba mengine ya ganda la dunia

Bamba hili limepakana na bamba la Karibi, bamba la Amerika ya Kaskazini, bamba la Afrika, bamba la Antaktika, bamba la Scotia na bamba la Nasca. Inawezekana ya kwamba limepakana na mabamba madogo mengine yasiyoeleweka bado.