Bamba la Afrika
Bamba la Afrika ni kati ya mabamba makubwa ya gandunia ya dunia yetu. Lipo chini ya bara la Afrika na chini ya sehemu za bahari zinazopakana nalo yaani tako la bara.
Bamba hili limepakana na bamba la Ulaya-Asia, bamba la Uarabuni, bamba la Uhindi, bamba la Australia, bamba la Antaktika na bamba la Amerika ya Kaskazini. Inawezekana ya kwamba limepakana na mabamba madogo mengine yasiyoeleweka bado.
Bamba la Afrika lina mwendo wa kuelekea kaskazini unaopimwa kuwa 2.15 cm kila mwaka. Kwa mkasi huu bara la Afrika litagusana na Hispania ya Kusini baada ya miaka 650,000 na kufunga mlango wa bahari ya Gibraltar hivyo kufunga Mediteranea na kuifanya kuwa ziwa.
Bamba la Afrika yenyewe liko katika mwendo wa kupasuliwa kwenye mstari wa ufa la Afrika ya Mashariki kutoka Eritrea kupitia Ethiopia, Kenya, Tanzania, Malawi na mwishowe katika Msumbiji. Sehemu mbili za bamba la Afrika huitwa na wataalamu bamba la Afrika ya Kinubia na la Afrika ya kisomalia.
![]() |
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|