Bamba la Antaktiki

(Elekezwa kutoka Bamba la Antaktika)

Bamba la Antaktiki ni bamba la gandunia linalobeba bara la Antaktiki na sehemu za sakafu ya bahari jirani.

Bamba la Antaktiki

Bamba hilo huwa na eneo la Km² 60,900,000.

Mabamba yanayopakana ni Bamba la Nazca, Bamba la Amerika ya Kusini, Bamba la Afrika, Bamba la Australia na Bamba la Pasifiki.

Kihistoria baada ya kuvunjika kwa Gondwana (sehemu ya kusini ya bara kuu la kale Pangaia, bamba la Antaktiki lilianza kusogea pale lilipo, kwenye ncha ya kusini ya dunia, na hivyo kusababisha tabianchi baridi kabisa ya Antaktiki. [1]

Tanbihi Edit