Barabara ya Julius K. Nyerere

Barabara ya Julius K. Nyerere (pia Nyerere Road) ni kati ya barabara kuu kwenye jiji la Dar es Salaam. Zamani ilijulikana zaidi kwa jina la Pugu Road maana inaelekea kutoka kitovu cha jiji kwenda Pugu upande wa kusini-magharibi.

Barabara hii inaanza kwenye njiapanda ya Gerezani Street inapita kituo cha reli ya Tazara na kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Inaendelea hadi Gongo la Mboto.

Kwenye njiapanda ya barabara ya Nyerere na barabara ya Nelson Mandela kuna daraja la Mfugale ambalo limesaidia kupunguza msongamano wa magari kwenye njiapanda hii.

Sehemu ya kwanza ya Pugu Road ya zamani siku hizi inaitwa Nkrumah Street.