Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar

jtedg

Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar ni bunge la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania inayojitawala katika mambo mengi ya ndani.[1]

Historia hariri

Baraza lilianzishwa mwaka 1980. Kabla ya mwaka huo, Baraza la Mapinduzi lilikuwa na shughuli za serikali na pia bunge kwa muda wa miaka 16 baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.[2]

Wabunge wa baraza hariri

Tangu uchaguzi wa mwaka 2020 baraza lina wabunge wafuatao:[3]

Aina ya Wajumbe tangu 2020 CCM ACT-W TADEA Jumla
Wajumbe wa kuchaguliwa majimboni 46 4 0 50
Wajumbe wa Kuteuliwa na Rais 4 2 1 7
Wajumbe Wanawake wa Viti Maalum 18 0 0 18
Spika 1 - - 1
Mwanasheria Mkuu - - - -
Jumla 69 6 1 76

Ilhali chama cha ACT-Wazalendo kilishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 19 za kura, kiliingia katika serikali ya umoja wa kitaifa kulingana na katiba ya Zanzibar.

Matokeo ya chaguzi za awali hariri

Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi kulikuwa na matokeo yafuatayo:[4]

Chama Mwaka wa uchaguzi
1995 2000 2005 2010 2015* 2016
Chama Cha Mapinduzi (CCM) 26 34 30 48 - 84
Civic United Front (CUF) 24 16 19 33 -
Wengine - - - - - 3
Jumla 50 50 50 82 - 88

Uchaguzi wa mwaka 2015 ulibatilishwa na mwenyekiti wa Tume la Uchaguzi la Zanzibar. Katika marudio ya mwaka 2016 chama cha CUF hakikukushiriki. "Wengine" katika bunge la 2016 walikuwa wajumbe walioteuliwa na rais, pamoja na mwanasheria mkuu aliyeingia kutokana na cheo chake.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. The Parliament of Zanzibar, Tanzania. Commonwealth Parliamentary Association. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-04-28. Iliwekwa mnamo 14 November 2014.
  2. History of the ZHoR. Zanzibar House of Representatives. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-11-29. Iliwekwa mnamo 15 November 2014.
  3. Baraza la kumi(2020-2025), uchambuzi wa kitakwimu wa aina za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Archived 24 Aprili 2021 at the Wayback Machine., tovuti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliangaliwa Aprili 2021
  4. Elections in Zanzibar. Iliwekwa mnamo 15 November 2014.

Viungo vya Nje hariri