Bass Sultan Hengzt
Fabio Ferzan Cataldi (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Bass Sultan Hengzt; amezaliwa 14 Agosti 1981) ni rapa kutoka nchini Ujerumani. Ana asili ya Kituruki/Kiitalia.
Bass Sultan Hengzt | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Fabio Ferzan Cataldi |
Amezaliwa | 14 Agosti 1981 |
Asili yake | Uturuki, Italia |
Aina ya muziki | Hip hop, gangsta rap |
Studio | Amstaff Muzx, Murderbass |
Ame/Wameshirikiana na | King Orgasmus One, MC Bogy, Fler, Sido, Mr. Long |
Tangu mwaka wa 2001, aliingia mkataba na studio ya I Luv Money Records akiwa kama mwanachama wa kundi la rap lililokuwa linachipukia Berlins Most Wanted (BMW) ambamo alifanya kazi pamoja na Bushido na King Orgasmus One. Ilivyofika mwaka wa 2003, akatoa albamu yake ya kwanza ya kujitegemea iliyokwenda kwa jina la Rap braucht kein Abitur, 2004 akatoa albamu iliyokwenda kwa jina la Bezirk zu Bezirk akiwa na MC Bogy.