Moses Ssali (amezaliwa 1 Septemba 1977) ni mwanamuziki wa ragga kutoka nchini Uganda. Anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Bebe Cool. Alianza kazi yake kutoka 1997 akiwa Nairobi, Kenya, lakini miaka michache baadaye alirudi nchini kwake. Pamoja na Nameless na mwenzake Chameleone, Bebe Cool alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza kujiimarisha na Ogopa DJs, nyumba ya uundaji muziki na studio nchini Kenya.

Nyimbo zake mbili maarufu ni "Fitina" na "Mambo mingi" [1] Yeye pia aliimba pamoja na Halima Namakula, msanii mwanamke kutoka katika wimbo wao "Sambagala". Alitoa albamu mbili, Maisha na Senta. Mistari ya nyimbo zake ziko katika Luganda, Kiswahili, na Kiingereza.

Bebe Cool ameshinda zawadi kadhaa katika Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) [2] Alikuwa ameteuliwa kwa Tuzo la Kora mwaka 2003 na 2005. Amezuru Uingereza na Marekani [3]

Pamoja na waimbaji wawili waKenya Necessary Noize, Bebe Cool ameunda kikundi cha reggae kinachojulikana kama East African Bashment Crew. Wametoa albamu moja, Fire, na nyimbo mbili, "Africa Unite" na "Fire". Kundi hili limeteuliwa katika uzinduzi wa (2008) MTV Africa Music Awards [4]

Bebe Kool ni mume wa aliyekuwa mshindani wa Miss Uganda Zuena Kirema na sasa ana watoto wawili.

Alishinda:

Ameteuliwa:

Marejeo

hariri

Viungo vya Nje

hariri