Nameless

Mwimbaji kutoka nchini Kenya

David Mathenge (amezaliwa Agosti 1976), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii Nameless, ni msanii wa kapuka nchini Kenya.

Taawasifu hariri

Yeye alipata umaarufu mwaka 1999 kupitia Ushindani wa "Star search" uliofanywa na stesheni ya radio ya [Capital(98.4 fm) http://www.capitalfm.co.ke], ambayo alishinda kwa wimbo wake wa awali "Megarider" Wimbo huu unaongelea m kijana ambaye hana pesa na ilhali anajaribu kumpata kipusa.Fedha alizonazo zinatosha tu tiketi ya Kenya Bus , na si maisha ambayo msichana huyo anataka. Alifanya wimbo huo na na mtayarishaji Tedd Josiah na ulikaa kwenya kwenye chati kwa wiki kadhaa Alitia saini na Ogopa Deejays mnamo mwaka wa 2001.katika Ogopa DJ's alikuwa pamoja na wasanii kama vile marehemu E-Sir amabaye walifanya wimbo wa "Boomba Train," na Amani : "Ninanoki" mwaka wa 2002 wimbo ambao ulivunja rekodi kwenya chati nchini Kenya kwa kusalia siku 110 nambari moja

Amekwenda kwenye ziara kaadhaa Afrika Mashariki , Marekani na pia Uingereza Alitoa albamu yake ya "on fire mwaka wa"2004. Pia mwaka huo huo wa 2004 Mathenge alimuoa msanii mwenzake Wahu Kagwe waliyekuwa wakirekodi pamoja katika Ogopa DJ's. Wana mtoto mmoja, binti ambaye alizaliwa mwaka 2006. Yeye pia ni mbunifu na alfuzu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

Kikundi cha 'pop' kutoka Afrika Kusini ; Jamali walitoa wimbon wimbo wa "nigger" na ilisemekana kwamba waliuiba wimbo huo kutoka kwa Nameless. Lakini baadaye Jamali walikubali kumshirikisha Nameless kama Mwandishi wa "maisha" kwenye albamu yao ya "Yours Fatally"

Yeye alikuwa miongoni mwa orodha ya watu mia moja (100) wenya ushawishi mkubwa sana nchini Kenya kama iliyotolewa na gazeti la The Standard Agosti 2007 [1][2]

Tuzo hariri

Kuchaguliwa hariri

Marejeo hariri

  1. The Standard, 21 Agosti 2007: 100 mest ushawishi Wakenya
  2. The Standard, 21 Agosti 2007: 100 mest ushawishi Wakenya - Entertainment
  3. Kisima Awards winners 2006. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-04-08. Iliwekwa mnamo 2009-11-26.
  4. Ugandaonline.net: PAM Awards 2006 Winners
  5. Tanzania Music Awards: 2007 winners Archived 2 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.
  6. Museke: Channel O Music Video Awards 2007 winners Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.
  7. Museke: PAM Awards Winners 2008 Archived 18 Aprili 2009 at the Wayback Machine.
  8. Kisima Music Awards: 2008 Kisima Music Awards Archived 12 Desemba 2009 at the Wayback Machine.
  9. Daily Nation, Buzz Magazine, 12 Aprili 2009: The Kilimanjaro Awards 2009: The Highs na Lows Archived 27 Februari 2012 at the Wayback Machine.
  10. Museke: MTV Africa Music Awards (MAMAs) 2009 winners
  11. Tanzania Music Awards - Nominees 2005. Jalada kutoka ya awali juu ya 2006-05-15. Iliwekwa mnamo 2006-05-15.
  12. Museke: MTV Africa Music Awards (MAMAs) 2009 nominees Archived 14 Oktoba 2009 at the Wayback Machine.

Viunganish vya nje hariri