Been There, Done That
"Been There, Done That" ni kibao cha mwaka wa 1997 kilichotolewa na rappa na matayarishaji wa West Coast Dr. Dre. Kibao kinatoka katika albamu yake ya vibao mchanganyiko ya Dr. Dre Presents the Aftermath. Wimbo umetayarishwa na Dr. Dre mwenyewe na Bud'da. Mashairi yalitungwa na mwanastudio mwenzake wa zamani wa Death Row Records, J-Flexx. Baada ya safari ya Dre kujitoa katika studiio hiyo - mwanastudio mwenzake J-Flexx ametoa kibao cha kuponda kwenye albamu ya vibao mchanganyiko ya Death Row Greatest Hits na kibao kilikwenda kwa jina la "Who Been There, Who Done That".
“Been There, Done That” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya Dr. Dre kutoka katika albamu ya Dr. Dre Presents the Aftermath | |||||
Imetolewa | 1997 (U.S.) | ||||
Muundo | CD | ||||
Imerekodiwa | 1996 | ||||
Aina | Hip hop | ||||
Urefu | 5:11 | ||||
Studio | Aftermath, Interscope | ||||
Mtunzi | Dr. Dre, Bud'da, J-Flexx | ||||
Mtayarishaji | Dr. Dre, Bud'da | ||||
Mwenendo wa single za Dr. Dre | |||||
|
Wimbo huu umetajwa mwishoni mwa kibao cha "Guilty Conscience" cha Eminem, ambacho kilikuwa kinaushirikiano na Dre.
Makala hii kuhusu wimbo wa hip hop bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |