Open main menu

Benard Michael Paul Mnyang’anga (amezaliwa tar. 8 Septemba, 1989) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya na mwigizaji kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ben Pol. Hasa anaimba muziki wa R&B. Ben Pol aiianza kuvuma mwaka 2010 baada ya kutoa kibao cha "Nikikupata" ambacho kiliweza kumtambulisha katika ulimwengu wa Bongo Flava. Baadaye akaja kutamba zaidi na kibao kama vile Samboira, Moyo Mashine, Jikubali, Namba One Fan, TATU, Sophia na nyingine kibao. Kiasili Ben ni mtu wa Dodoma.[1] Tena anajisifu kama mtu kutoka kanda ya kati Dodoma. Kwa upande filamu, amepata kucheza katika filamu ya Sunshine na baadhi tu ya filamu zilizokuwa chini ya MFDI Tanzania na kuongozwa na Karabani.[2]

Ben Pol
Jina la kuzaliwa Benard Michael Paul Mnyang’anga
Pia anajulikana kama Ben Pol
Amezaliwa 8 Septemba 1989 (1989-09-08) (umri 30)
Kazi yake Mwimbaji
Mwigizaji
Ala Sauti
Miaka ya kazi 2009-hadi sasa
Ameshirikiana na Darassa, Saida Karoli, Belle 9

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  1. Ben Pol katika Bongo Swaggz
  2. Sunshine "Ben Pol akicheza kama m-bwia unga".
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ben Pol kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.