Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

bendera ya taifa

Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepatikana tangu Februari 2006 kutokana na katiba mpya ya nchi. Katiba iliazimia kurudia mfano wa bendera iliyowahi kutumiwa kati ya miaka 1963 na 1971 kabla nchi haijaitwa "Zaire". Buluu yake imebadilishwa kuwa buluu ya angani sawa na bendera ya uhuru ya mwaka 1960.

Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu mwaka 2006.
Bendera ikipeperuka.

Buluu ya bendera inakatwa na mlia wa hanamu wenye rangi nyekundu na ya dhahabu. Nyekundu ilimaanisha damu ya mateso chini ya ukoloni na mapambano kwa ajili ya uhuru. Dhahabu ilikumbusha juu ya utajiri wa nchi. Nyota ya rangi ya dhahabu iko kwenye pembe ya juu jinsi ilivyokuwa katika bendera za Kongo tangu ukoloni.