Benki ya Maendeleo ya TIB

Benki ya Maendeleo ya TIB (mwanzo ilijulikana kama Benki ya Uwekezaji Tanzania, TIB), ni benki ya maendeleo inayomilikiwa na serikali nchini Tanzania. Benki hiyo ni taasisi ya kwanza ya fedha ya maendeleo iliyoanzishwa na Serikali ya Tanzania. Shughuli za TIB zinasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania, benki kuu na mdhibiti wa kitaifa wa benki. TIB imesajiliwa kama Taasisi ya Fedha Iliyosajiliwa.

Historia hariri

Benki hiyo ilianzishwa na Sheria ya Bunge mnamo mwaka 1970. Wakati huo, lengo kuu la TIB lilikuwa kutoa "mikopo ya muda wa kati na muda mrefu kwa wawekezaji katika sekta ya kilimo biashara, utengenezaji, usindikaji, ujenzi, uchukuzi, utalii na madini". Hata hivyo, kutokana na ugumu wa kiuchumi, pamoja na Vita vya Kagera dhidi ya Idi Amin wa nchi jirani ya Uganda na mabadiliko ya ubadilishaji wa fedha za kigeni ndani ya uchumi wa Tanzania, benki hiyo ilishindwa kutekeleza majukumu yake ya kifedha. Ili kupunguza hasara za kifedha, TIB iliamua kutoa mikopo ya muda mfupi na kufanya kazi kama benki ya biashara. Kipindi kati ya mwaka 1980 hadi mwaka 2003 kilikuwa kigumu sana kwa benki.

Maendeleo Taasisi ya Fedha hariri

Baada ya muda, serikali ya Tanzania, iliipa tena benki hiyo, iliyoboresha mipango yake ya maendeleo ya kimkakati na kupanga upya usimamizi wake. Kuanzia Desemba mwaka 2010, TIB ilikuwa na jumla ya mali zaidi ya Dola za Marekani milioni 62 (TZS: bilioni 93). Serikali inakusudia kuongeza idadi hiyo hadi Dola za Marekani milioni 265 (TZS: 400 bilioni), katika miaka kadhaa ijayo. Benki ina sehemu kubwa ya jalada lake katika sekta ya kilimo ya Tanzania.

Matawi hariri

Benki hii ina matawi katika maeneo yafuatayo:

1.Tawi la Dar es salam - Barabara ya Sam Nujoma, Mlimani City jengo la tatu,Dar_es_Salaam
2.Tawi la Mwanza - jengo la PPF Plaza Ghorofa ya tatu, Mwanza
3.Tawi la Arusha - Barabar ya Sokoine, Jengo la Central Plaza, Arusha
4.Tawi la Mbeya - Mbeya, Mtaa wa Jakaranda 28
5.Tawi la Dodoma - Dodoma
6.Tawi la Zanzibar - Zanzibar

Marejeo hariri