Benki Kuu ya Tanzania

Benki Kuu ya Tanzania ni benki ya kitaifa inayosimamia masuala ya kibenki na kifedha nchini Tanzania. Makao yake makuu yako Dar es Salaam.

Benki Kuu ya Tanzania katika Dar es Salaam

Kati ya majukumu yake ni utoaji wa fedha za Tanzania, Shilingi ya Tanzania.

Benki Kuu ya Tanzania iliundwa na Sheria ya Benki ya Tanzania 1965.

Mwaka 1995, baada ya kuonekana kuwa benki hii ina majukumu mengi kuzidi uwezo wake, Sheria ya Benki ya Tanzania 1995 ilipitishwa na kuipa benki hii jukumu moja ambalo ni kusimamia sera ya fedha nchini.

Benki hii huongozwa na Bodi ya Wakurugenzi yenye wajumbe kumi.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Benki Kuu ya Tanzania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.