Bethsaida
Bethsaida (kutoka Kiebrania/Kiaramu בית צידה beth-tsaida, yaani "Nyumba ya uwindaji" au "ya uvuvi", kutoka mzizi צדה auצוד)[1] ni mahali panapotajwa na Agano Jipya.
Palikuwa upande wa mashariki wa mto Yordani, labda jirani na mahali ambapo mto huo unaingia katika Ziwa Galilaya. [2]
Bethsaida ndio mji asili wa mitume wa Yesu wafuatao: Petro, Andrea nduguye na Filipo (Yoh 1:44).
Bethsaida inatajwa na Mk 8:22-26 kama mji (κώμη) ambapo Yesu alimponya kwa awamu mbili mwanamume kipofu.
Ingawa katika Injili hakuna habari za miujiza mingine iliyofanyika huko, Yesu aliutishia mji huo laana ya milele kwa kutopokea ujumbe wake wa toba.
Tanbihi
hariri- ↑ https://www.biblicaltraining.org/library/bethsaida-beth-saida
- ↑ (Ant., XVIII, ii, 1; BJ, II, ix, 1; III, x, 7; Vita, 72)
Marejeo
hariri- Arav R and RA Freund (2004) Bethsaida: A City by the North Shore of the Sea of Galilee Truman State University. ISBN 978-1-931112-39-0.
- Bethsaida: An Ancient Fishing Village on the shore of the Sea of Galilee , 2001, Israel Ministry of Foreign Affairs.
- International Standard Bible Encyclopedia
Viungo vya nje
hariri- Bibleplaces.com Bethsaida Ilihifadhiwa 22 Desemba 2012 kwenye Wayback Machine.
- Bethsaida, by Jacqueline Schaalje
- Strong's G966 Ilihifadhiwa 13 Agosti 2016 kwenye Wayback Machine.
- The Secrets of Bethsaida, a documentary by Yuval Hollander Ilihifadhiwa 19 Agosti 2013 kwenye Wayback Machine.
32°54′36″N 35°37′52″E / 32.910°N 35.631°E
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bethsaida kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |